• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Kenya kupimwa na Uganda, Afrika Kusini kwenye riadha za kitaifa Juni 22

Kenya kupimwa na Uganda, Afrika Kusini kwenye riadha za kitaifa Juni 22

NA AYUMBA AYODI

WANARIADHA kutoka mataifa ya Afrika Kusini, eSwatini, Ushelisheli, Uganda, Sudan Kusini na Tanzania wamethibitisha kushiriki mashindano ya kitaifa yatakayofanyika ugani Nyayo hapo Juni 22-24.

Afisa Mkuu Msimamizi wa Shirikisho la Riadha Kenya (AK) Susan Kamau amesema kuwa wanariadha wengi wa kigeni watashiriki mbio fupi pamoja na zile za kupokezana vijiti za wanaume za mita 4×400 na 4x100m.

Amefichua kuwa riadha hizo zimevutia wanariadha wa kigeni kwa sababu ni mojawapo ya mashindano machache yanayotambuliwa na Shirikisho la Riadha Duniani na wanariadha wanaweza kufuzu kushiriki Riadha za Dunia mnamo Agosti 19-27 jijini Budapest, Hungary.

Kamau amesema kuwa Kenya ina fursa nzuri ya kufuzu katika mbio za wanaume za 4x400m na 4x100m kupitia viwango bora duniani ikiwa itafanya vyema kwenye kiwango hicho cha kitaifa.

Sheria za Shirikisho la Riadha Duniani zinasema kuwa mataifa angaa matatu yanahitaji kushindana katika mashindano ya kupokezana vijiti ili yapate kuorodheshwa duniani.

“Tunalenga kuingiza vikosi imara katika vitengo vyote viwili ili kuwa na fursa nzuri ya kufuzu kupitia viwango vya ubora duniani,” amesema.

Kamau pia amesema kuwa mashindano ya kitaifa inatoa nafasi nzuri kwa wanariadha ambao hawajatimiza viwango vya kufuzu kufanya hivyo.

“Tutatumia pia mashindano ya kitaifa kuchagua wanariadha watakaoshiriki mchujo wa kitaifa utakaofanyika Julai 7-8 na wala sio Julai 14-15 ilivyotangazwa hapo awali.

Kamau amefafanua kuwa wataandaa mchujo mapema ili kuwapa wanariadha muda mzuri wa kushiriki mashindano kadhaa ya Diamond League kabla ya Budapest na shughuli ya kupata Visa.

Mashindano hayo ya Diamond League ni Silesia mnamo Julai 16 nchini Poland, Monaco (Julai 21) na London (Julai 23).

TAFSIRI: GEOFFREY ANENE  

  • Tags

You can share this post!

AMINI USIAMINI: Tandu wanaofahamika kama Giant centipedes

Wahalifu wajificha kwa makundi yanayofika hospitalini...

T L