• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 7:15 PM
Kimanzi aibuka kocha bora wa Januari 2021 Ligi Kuu ya Kenya

Kimanzi aibuka kocha bora wa Januari 2021 Ligi Kuu ya Kenya

Na GEOFFREY ANENE

FRANCIS Kimanzi ndiye kocha bora wa Ligi Kuu ya Kenya wa mwezi Januari.

Kocha huyo mkuu wa klabu ya Wazito aliongoza mabwanyenye hao kuzoa ushindi mara tano mwezi Januari, mafanikio ambayo yaliwainua hadi nambari tatu kwenye jedwali mwisho wa mwezi huo.

Kimanzi, ambaye alijiunga na Wazito baada ya kutemwa na timu ya taifa ya Harambee Stars, aliibuka kocha bora wa Januari baada ya kumpiku Robert Matano (Tusker FC) ambaye aliandikisha ushindi mara nne na kupiga sare moja mnamo Januari.

Wanamivinyo wa Tusker wako juu ya jedwali wakati huu.

Wazito walifungua mwaka 2021 kwa kuzaba Nairobi City Stars 2-1 uwanjani Utalii Grounds kabla ya kunyamazisha AFC Leopards 1-0 na Bidco United 2-1 uwanjani humo.

Michuano yake miwili ya mwisho ya Januari ilihamishiwa Kasarani, lakini mabadiliko hayo ya uwanja hayakuzuia Wazito kuendeleza ukatili wake ilipocharaza Nzoia Sugar 2-1 kabla ya kulima Kakamega Homeboyz 1-0.

Tuzo hiyo huandamana na Sh50,000 na kombe kwa mshindi kutoka kwa Ligi Kuu.

Kimanzi ni kocha wa pili kupokea tuzo hiyo  baada ya kocha wa KCB FC, Zedekiah “Zico” Otieno aliyefungua msimu kwa kuibuka bora mwezi Desemba.

Washindi tuzo ya mwezi huchaguliwa na paneli la waandishi chini ya Ligi Kuu na Chama cha Wanahabari wa michezo (SJAK).

You can share this post!

Obiri kutumia tuzo ya Forbes kama kichocheo cha kuonyesha...

Wapepetaji wakuu wa Covid