• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:55 AM
Kipng’eno na Njeru watawala mbio za milimani Austria

Kipng’eno na Njeru watawala mbio za milimani Austria

Na GEOFFREY ANENE

WAKENYA Patrick Kipng’eno na Joyce Njeru walifagia mataji ya mbio za milimani za Grossglockner Berglauf mjini Austria, Jumapili.

Katika mbio hizo za nne za Kombe la Dunia la Valsir alikamilisha mbio za kilomita 13 kwa dakika 68 na sekunde 22 akifuatiwa na Wakenya wenzake Philemon Kiriago (70:03) na Petro Mamu (70:05) mtawalia.

Njeru alitwaa taji la akina dada baada ya kukata utepe kwa dakika 85:56.

Mkenya Lucy Murigi aliridhika na nafasi ya pili kwa 88:28 naye Adela Stranska kutoka Jamhuri ya Czech akafunga watimkaji tatu-bora kwa 90:21.

Mshindi wa duru ya kufungua msimu mjini Montemuro nchini Ureno, Kipng’eno ni bingwa wa mbio za milima nchini Kenya.

Njeru alikuwa akitetea taji la Grossglockner Berglauf. Murigi ni bingwa wa dunia mwaka 2017 na 2018. Mbio za Grossglockner Berglauf 2022 ni makala ya 22. Njeru sasa ana alama 100. Amekaa juu ya jedwali la mbio za milimani za Kombe la Dunia la Valsir.

Kipng’eno pia anafurahia uongozi wa kitengo cha wanaume kwa alama 100. Duru ijayo ni La Montee du Nid d’Aigle nchini Ufaransa mnamo Julai 16.

  • Tags

You can share this post!

Wawaniaji 3 washinda viti bila kupingwa na yeyote

MKU yazindua kituo kipya cha utafiti na ubunifu

T L