• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Wawaniaji 3 washinda viti bila kupingwa na yeyote

Wawaniaji 3 washinda viti bila kupingwa na yeyote

NA MERCY CHELANGAT

MGOMBEAJI mmoja wa kiti cha Mwakilishi wa Kike, na wawili wa udiwani wametangazwa washindi bila jasho baada ya kukosa wapinzani.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Jumapili ilimtangaza Beatrice Kemei, mgombea wa kiti hicho katika kaunti ya Kericho kwa tiketi ya chama cha United Democratic Alliance (UDA) kuwa mbunge.

Wanaume wawili ambao ni wagombeaji wa udiwani katika kaunti za Garissa na Baringo pia wamepata ushindi wa moja kwa moja.

Bi Kemei alimshinda mshikilizi wa wadhifa huo sasa katika uchaguzi wa mchujo uliofanyika Aprili 14, 2022.

Kemei alizoa jumla ya kura 87,182 huku Bi Bore akipata kura 64,651.

Wanaume ambao wamepokezwa ushindi wa udiwani ni Issa Abdi wa wadi ya Sabena (Garissa) na Julius Kimutai wa wadi ya Ravine (Baringo).

Bw Kimutai pia aliwania kwa tiketi ya chama cha UDA huku Bw Abdi akiwa amedhamiwa na chama cha National Agenda Party of Kenya (NAPK).

Watatu hao wamejiunga katika orodha ya viongozi ambao wamewahi kuchaguliwa bila kupingwa katika chaguzi za majuzi.

Wao ni mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung’wa (2017) na mwenzake wa Gatundu Kusini Moses Kuria (2013).

You can share this post!

Kindiki, Muturi walalama Uhuru hana shukurani

Kipng’eno na Njeru watawala mbio za milimani Austria

T L