• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Kocha Graham Potter hatarini

Kocha Graham Potter hatarini

Na MASHIRIKA

LONDON, Uingereza

HUENDA kocha Graham Potter akafutwa kazi leo Alhamisi usiku iwapo Chelsea watachapwa na Fulham kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Premia (EPL) itakayochezewa Craven Cottage.

Kulingana na bodi ya klabu hiyo, kocha huyo mwenye umri wa miaka 47 amepewa muda wa kutosha kurekebisha kikosi chake, lakini hawaoni mabadiliko yoyote tangu achukue usukani kutoka kwa Thomas Tuchel mwezi Septemba 2022.

Baada ya matokeo mabaya yaliyofuatana, kocha alitetewa na wenzake akiwemo Pep Guardiola aliyedai kwamba yuko katika utaratibu wa kujenga kikosi chake.

Potter anapitia wakati mgumu kama kocha hasa baada ya kuywa na msururu wa matokeo mabaya tangu ligi iliporejelea baada kumalizika kwa fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar.

Chelsea ilikutana na Manchester City katika mechi ya ligi na kulazwa 1-0 kabla ya Jumapili iliyopita kucharazwa 4-1 na vigogo hao wa Etihad katika pambano la FA Cup.

Straika wa Manchester City raia wa Argentina Julian Alvarez akifunga bao kupitia penalti wakati wa mechi ya FA raundi ya tatu dhidi ya Chelsea uwanjani Etihad mnamo Jumapili.

Kutokana na matokeo hayo, mashabiki wa klabu hiyo wameanza kumfokea kocha huyo wakimtaka aondoke, lakini anazidi kutetewa na baadhi ya mashabiki wanaodai uongozi wa klabu ndio duni, tangu kuondoka kwa Abramovich.

“Najua katika timu kubwa, matokeo ni mihimu, lakini ningependa apewe muda zaidi,” alisema Guardiola.

Chelsea ambao wamepata ushindi mmoja tu katika mechi nane wanashikilia nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi kuu, pointi 10 kutoka nafasi ya Nne Bora ambayo inawezesha timu kufuzu kwa Kombe la Klabu Bingwa barani Ulaya, na pointi 10 kutoka eneo la hatari la kushishwa daraja.

Fulham wako katika kiwango kizuri kwa sasa, ambapo tangu kumalizika kwa Kombe la Dunia wameandikisha ushindi dhidi ya Crystal Palace, Southampton na Leicester City ligini.

Kadhalika, waliibuka na ushindi dhidi ya Hull City katika pambano la FA Cup mwishoni mwa wiki. Lakini, Chelsea wanajivunia ushindi mara saba mfululizo dhidi ya Fulham.

  • Tags

You can share this post!

KINYUA BIN KING’ORI: Ruto, Raila wasitusumbue...

Jinsi programu ya ‘Ponea Patient’ inavyosaidia...

T L