• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 8:03 AM
Kocha Lennon ayoyomea Cyprus kudhibiti mikoba ya Omonia Nicosia

Kocha Lennon ayoyomea Cyprus kudhibiti mikoba ya Omonia Nicosia

Na MASHIRIKA

KOCHA wa zamani wa Celtic, Neil Lennon, ameteuliwa kuwa mkufunzi wa klabu ya Omonia Nicosia inayoshiriki Ligi Kuu ya Cyprus.

Lennon ambaye ni raia wa Northern Ireland ametia saini mkataba utakaomshuhudia akihudumu kambini mwa Nicosia hadi mwisho wa msimu wa 2023-24.

Amekuwa nje ya ulingo wa ukocha tangu Februari 2021 alipojiuzulu katika akihudumu kwa awamu ya pili kama mkufunzi wa Celtic.

Omonia Nicosia waliajiri Lennon ili kujaza pengo la mkufunzi Henning Berg ambaye ni beki wa zamani wa Rangers na Manchester United. Kikosi hicho kilibanduliwa mapema kwenye soka ya Europa Conference msimu huu.

Lennon, 50, aliongoza Celtic kuzoa mataji 10 ya haiba kubwa katika awamu mbili za ukufunzi wake ambapo alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu ya Scotland, makombe mawili ya Scottish Cups na ubingwa wa League Cup. Alirejea kambini mwa kikosi hicho kwa awamu ya pili mnamo Februari 2019 baada ya kocha Brendan Rodgers kukubali mikoba ya Leicester City nchini Uingereza.

Lennon amewahi pia kudhibiti mikoba ya ya Bolton Wanderers na Hibernian katika Ligi Kuu ya Scotland mnamo 2017.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Klopp ataka Liverpool kujihadhari dhidi ya Inter Milan...

KYSD Soccer Stars, Kinyago mtazikoma hakuna kuzaa

T L