• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 5:50 PM
Kocha: Prisons tupo ngangari kukabili wapinzani wetu

Kocha: Prisons tupo ngangari kukabili wapinzani wetu

Na JOHN KIMWERE

KOCHA wa timu ya wanawake ya Kenya Prisons, Josp Baraza amesema wapinzani wao wameimarisha mchezo wao lakini hilo halitamtia hofu kwenye juhudi za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Shirikisho la Voliboli nchini (KVF) msimu huu.

Anasema kuwa licha ya kutosaini wachezaji wa nguvu anaamini kikosi chake kinatosha mboga kukabili washindani wao. Wapinzani wao Kenya Pipeline, timu ya Maafisa wa Uchunguzi wa Jinai (DCI) na KCB kila moja ilisaini wachezaji kadhaa tayari kujiweka imara kuwania taji la muhula huu.

Kutokana na hilo kocha huyo anakiri kuwa anatarajia upinzani mkali kwenye kampeni za msimu huu. ”Kamwe sina shaka na wachezaji wangu kwa kuzingatia nina warembo wazuri waliohifadhi ubingwa wa ligi muhula uliyopita,” alisema na kuongeza kuwa wanaendelea na mazoezi kujiandalia mechi za mkondo wa pili zitakaoandaliwa jijini Mombasa.

Anapongeza vipusa wake akiwamo Rebecca Mwendwa, Mcline Akoko na Naomi Wekesa kwa kuimarisha mchezo wao kinyume na msimu uliyopita. Pipeline inajivunia kusaini upya Noel Murambi na Violet Makuto kutoka KCB. Pia ilitwaa huduma za Veronica Oluoch na Carolyne Serengo wote kutoka (DCI) bila kuweka katika kaburi la sahau Daisy Chepkorir kutoka shule.

Nayo DCI ilinasa huduma za mvamizi Sharon Chebet na Vivian Bor kutoka Cheptil Girls na New Light Academy mtawalia. Pia ilisaini Faith Oilakin kutoka Chuo cha Kenyatta (KU) na Gladys Wairimu aliyekuwa akichezea Nairobi Water.

You can share this post!

TUSIJE TUKASAHAU: Umaskini na ukosefu wa intaneti...

Ruto alaani mswada wa mageuzi ya sheria ya uchaguzi

T L