• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:55 AM
Kocha wa  DCI anapongeza vipusa wake kwa kujituma mazoezini

Kocha wa DCI anapongeza vipusa wake kwa kujituma mazoezini

Na JOHN KIMWERE

KOCHA wa timu ya voliboli ya wanawake ya Maafisa wa Uchunguzi wa Jinai (DCI), Daniel Bor anasema wachezaji wake wanazidi kuimarika mazoezini ambapo atakuwa na kibarua kigumu kuteua kikosi kitakachoshiriki mechi za ligi wiki ijayo.

”Ninapongeza wachezaji wangu kwa bidii wanayotia mazoezini kujiweka tayari kushiriki mechi za mkondo wa pili wiki ijayo,” kocha huyo alisema na kuwataka wazidi kukaza buti maana wanataka tiketi ya kushiriki fainali za mwaka huu. Alidokeza kuwa kiasi wasiwasi umepungua kwa kuzingatia kabla ya mwanzo wa msimu huu alipoteza wachezaji watano waliokuwa tegemeo kwa kikosi chake.

Kikosi hicho kilipoteza huduma za Marion Indeche (mvamizi wa kulia), Faith Imodia (seta) na Libero Josphine Wafula wote walijiunga na KCB ya kocha, Japheth Munala. Nao Caroline Sirengo na Veronica Adhiambo walisajiliwa na Kenya Pipeline ya kocha, Paul Gitau. ”

Kusema ukweli inaumiza maana nimenoa makucha ya wachezaji wangu kwa muda kisha wakati wameiva tu huku nikitarajia watasaidia kwenye mechi za ligi wanashawishiwa na hela na kuhama,” alisema na kuongeza kuwa ina maana klabu inaweza kupoteza wachezaji wake kwa wakati mmoja.

DCI inashiriki Ligi Kuu ya Shirikisho la Voliboli ya Kenya (KVF) bila kuweka katika kaburi la sahau Kenya Pipeline, Kenya Prisons na KCB kati ya zingine.

 

You can share this post!

Kinara wa zamani wa NSSF na wakuu wa kampuni ya hisa...

Beki Calum Chambers aondoka Arsenal na kutua Aston Villa

T L