• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 2:00 PM
Leicester wasuka upya safu yao ya uvamizi kwa kusajili fowadi Mateus Tete wa Brazil kutoka Lyon

Leicester wasuka upya safu yao ya uvamizi kwa kusajili fowadi Mateus Tete wa Brazil kutoka Lyon

Na MASHIRIKA

LEICESTER City wamejinasia huduma za fowadi Mateus Tete kutoka Shakhtar Donetsk ya Ukraine hadi Juni 2023.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa akichezea Olympique Lyon ya Ufaransa kwa mkopo tangu Machi 2022 kabla ya mkataba wake kusimamishwa kwa muda na Shakhtar kufuatia agizo la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

FIFA iliwahi kutoa idhini kwa vikosi vya Ukraine kusitisha kandarasi za wanasoka wa kigeni hadi Juni 30, 2023 baada ya taifa hilo kuvamiwa na Urusi.

Tete amechezea Lyon jumla ya mechi 30 na kupachika wavuni mabao manane huku akichangia mengine 10. Hata hivyo, alikuwa bado na mkataba na Shakhtar hadi mwisho wa Julai 2023.

Kufikia sasa, Leicester wanakamata nafasi ya 14 kwenye msimamo wa jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) japo ni alama moja pekee ambayo inawatenganisha na vikosi vitatu vya mwisho jedwalini.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Knut yakosoa serikali kurukia Gredi ya 7, 8 na 9

Musalia Mudavadi atawazwa mlezi wa Baraza la Wazee

T L