• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Lewandowski aweka rekodi ya ufungaji katika mechi za Bundesliga

Lewandowski aweka rekodi ya ufungaji katika mechi za Bundesliga

Na MASHIRIKA

ROBERT Lewandowski aliweka rekodi ya kufunga bao katika kila mchuano wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) kwa mara ya saba mfululizo mnamo Ijumaa.

Hata hivyo, waajiri wake Bayern Munich wanaotiwa makali na kocha Julian Nagelsmann waliambulia sare ya 1-1 katika mchuao huo uliowakutanisha na Borussia Monchengladbach.

Alassane Plea aliwaweka Gladbach kifua mbele katika dakika ya 10 baada ya kuadaliwa pasi safi na Lars Stindl. Hata hivyo, Lewandowski alisawazisha mambo mwishoni mwa kipindi cha kwanza baada ya kushirikiana vilivyo na Joshua Kimmich.

Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Bayern ambao wamenyanyua taji la Bundesliga katika misimu tisa iliyopita mfululizo kutokuwa wa kwanza kufunga bao katika gozi la ufunguzi wa msimu mpya kweny Bundesliga tangu 2012.

Nusura Lewandowski ambaye ni nahodha wa Poland afungie Bayern bao la ushindi mwishoni mwa kipindi cha pili.

Nyota huyo ametikisa nyavu za wapinzani katika kila mojawapo ya mechi 11 zilizopita za Bundesliga na kujivunia jumla ya magoli 18. Mara ya mwisho kwa Lewandowski kuchezea Bayern bila kufunga bao ilikuwa Februari 2021.

Hadi walipofungua kampeni za msimu huu wa 2021-22, Bayern hawakuwa wamesajili ushindi wowote katika michuano ya kujiandaa kwa muhula mpya chini ya Nagelsmann aliyeagana na RB Leipzig mwishoni mwa muhula wa 2020-21.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Uhuru, naibu wake wasuka njama ya kuangusha waasi

Wakazi wataka Rais aepuke siasa za urithi