• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 6:50 AM
Macho yote kwa Shujaa,Morans Safari 7s ikianza

Macho yote kwa Shujaa,Morans Safari 7s ikianza

Na GEOFFREY ANENE

WENYEJI Kenya watakuwa mawindoni wakidiriki kuanza vyema mashindano ya kimataifa ya raga ya wachezaji saba kila upande ya Safari Sevens jijini Nairobi ugani Nyayo, leo.

Kenya inawakilishwa na wafalme wa mwaka 2000, 2013 na 2016 Shujaa, na mabingwa watetezi Morans pamoja na timu ya chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 maarufu kama Chipu.Washindi wa raga ya wachezaji saba kila upande nchini, KCB pia wako katika orodha ya timu 12 zitakazowania ubingwa.

Kocha Innocent Simiyu alitaja kikosi chake cha Shujaa kilicho na mchanganyiko wa wachezaji wazoefu akiwemo Alvin “Buffa” Otieno pamoja na wapya kama Collins Shikoli.Paul Murunga, ambaye anatia makali Morans, anajivunia kuwa na huduma za mchezaji mzoefu Augustine Lugonzo.

Nyota Collins Injera na Andrew Amonde wako katika kikosi cha Samurai International kilichoshinda mataji ya 2015 na 2018.Nayo Red Wailers ina mzoefu Leonard Mugaisi. Samurai na Wailers zinatoka Uingereza.

Zinaunda timu kwa kukusanya wachezaji kutoka mataifa mbalimbali. Chipu imetaja kikosini mwake Gabriel Ayimba ambaye ni mtoto wa kocha na mchezaji wa zamani wa Kenya, mwendazake Benjamin Ayimba.

Timu nyingine kali zinazoshiriki Safari Sevens katika kitengo cha wanaume ni Uhispania, Ujerumani, Uganda na Zimbabwe. Kenya na Uhispania zinatumia mashindano haya kujiandaa kwa msururu wa Raga ya Dunia makala ya 2021-2022 yatakayoanza Novemba 26-27 jijini Dubai.

Shujaa, leo, itaanza kampeni dhidi ya washiriki wapya Stallions kutoka Nigeria nayo Morans itapimwa vilivyo na Uganda.Mashindano haya ya siku mbili pia yatashuhudia Kenya Lionesses ikiwania taji la kinadada dhidi ya Titans kutoka Afrika Kusini, Uganda na Zimbabwe.

You can share this post!

FC Barcelona katika mizani ya Alaves La Liga ikimsubiri Xavi

Polisi wasaka ngariba kwa kuwakeketa wanawake

T L