• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 3:46 PM
Man-City wapewa mswaki katika makundi ya UEFA

Man-City wapewa mswaki katika makundi ya UEFA

Na MASHIRIKA

HUKU Newcastle United wakipewa miamba wa haiba katika hatua ya makundi ya gozi la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA), Manchester wanapigiwa upatu wa kutinga kirahisi raundi ya muondoano.

Mabingwa hao watetezi wa UEFA, wametiwa katika Kundi G pamoja na RB Leipzig ya Ujerumani, Young Boys ya Uswisi na Red Star Belgrade ya Serbia iliyonyanyua taji la European Cup mnamo 1991.

Arsenal wamerejea katika kivumbi cha UEFA kwa mara ya kwanza tangu 2016-17 na wametiwa katika Kundi B pamoja na PSV Eindhoven ya Uholanzi, RC Lens ya Ufaransa na wafalme wa Europa League, Sevilla, kutoka Uhispania.

Manchester United wametiwa katika Kundi A pamoja na mabingwa wa Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga), Bayern Munich, katika pambano litakalorejesha kumbukumbu za fainali ya UEFA 1999. Kundi hilo linajumuisha pia FC Copenhagen ya Denmark na Galatasaray kutoka Uturuki.

Kundi E lina Atletico Madrid, Celtic, Lazio na wafalme wa Ligi Kuu ya Uholanzi (Eredivisie), Feyenoord.

Man-United watakutana na nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza, Harry Kane, ambaye kwa sasa anasakatia Bayern baada ya kukatiza uhusiano wake na Tottenham Hotspur muhula huu. Nao wanatarajiwa kuwa na nafasi maridhawa ya kusonga mbele ikizingatiwa ‘unyonge’ wa Copenhagen na Galatasaray.

Timu nyingine inayotarajiwa kuwa na wakati mgumu wa kufuzu kwa hatua ya muondoano ni Arsenal hasa ikizingatiwa ubabe wa PSV Eindhoven na Sevilla ambao ni magwiji wa kutwaa mataji ya Europa League.

Newcastle walirejea katika soka ya UEFA muhula huu, kwa mara ya kwanza tangu 2002-03. Walijikatia tiketi hiyo ya UEFA baada ya kuambulia nafasi ya nne katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo 2022-23.

Mtihani wao mgumu zaidi unatazamiwa kuwa dhidi ya Dortmund, PSG walionogesha fainali ya 2020 na mabingwa mara saba AC Milan walipigwa 1-0 na Man-City katika fainali ya 2022-23. Dortmund ya Ujerumani ilinyanyua taji la UEFA mnamo 1997 na walifuzu kwa fainali ya kivumbi hicho miaka 10 iliyopita.

Mechi za hatua ya makundi zimeratibiwa kutandazwa kati ya Septemba 19 na Disemba 13, 2023 huku fainali ya UEFA ikitarajiwa kufanyika ugani Wembley, Uingereza, mnamo Juni 1, 2024.l

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Hatukuidhinisha mtambo wa Worldcoin wa kumulika macho...

Aliyekuwa afisa wa NMS asimulia machungu ya maisha

T L