• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Hatukuidhinisha mtambo wa Worldcoin wa kumulika macho – Chiloba

Hatukuidhinisha mtambo wa Worldcoin wa kumulika macho – Chiloba

NA CHARLES WASONGA

UCHUNGUZI wa Tume ya Mawasiliano Nchini (CA) umebaini kuwa kampuni tata ya Worldcoin iliingiza nchini mitambo ya kukusanya data za kibinafsi kutoka kwa Wakenya kabla ya kusaka idhini ya awali kutoka kwa tume hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa CA Ezra Chiloba mnamo Alhamisi aliambia kamati ya bunge inayochunguza shughuli za kampuni hiyo nchini kwamba mtambo huo kwa jina ‘Orb’ na ambao kumulika macho, haukuidhinishwa na tume yake.

“Hatuna rekodi yoyote ya kuonyesha kuwa kifaa hicho cha Orb kiliidhinishwa na Tume ya Mawasiliano Nchini. Kile kinachohitajika kufanyika ni kwamba ukiagiza kifaa kama hicho cha kukusanya data, sharti utume maombi ya uidhinishwaji ili baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege unapewa cheti cha kukuruhusu kifaa kitumike nchini,” Chiloba akaeleza.

Mkurugenzi huyo Mkuu alisema hayo alipofika mbele ya kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Narok Magharibi Daniel Tongoyo katika ukumbi wa County, Nairobi.

Imefichuka kuwa kwa kufeli kushirikiana na asasi zingine kudhibiti kampuni ya Tools for Humanity, kampuni ambayo Worldcoin ilitumia kuingia nchini na kuanzisha shughuli za kukusanya data nchini.

Worldcoin iliahidi kulipa Sh7,000 kwa kila mmoja wa maelfu ya Wakenya waliojitokeza kupeana data zao kwa kumulikwa macho. Ahadi hiyo ilivutia maelfu ya watu hawa wale walalahoi ambao walifurika katika uwanja wa jumla wa mikutano katika ukumbi wa KICC, Nairobi wakitaka kusajiliwa katika mradi huo.

  • Tags

You can share this post!

Mshukiwa wa uhalifu anayerejelewa kama ‘mzee wa...

Man-City wapewa mswaki katika makundi ya UEFA

T L