• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 5:50 AM
Man-United na Palace watoshana nguvu kwa sare ya 1-1 katika EPL ugani Selhurst Park

Man-United na Palace watoshana nguvu kwa sare ya 1-1 katika EPL ugani Selhurst Park

Na MASHIRIKA

MANCHESTER United walipoteza alama muhimu katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) baada ya Crystal Palace kuwalazimishia sare ya 1-1 mnamo Jumatano usiku ugani Selhurst Park.

Wenyeji Palace walisawazisha kupitia kwa Michael Olise mwishoni mwa kipindi cha pili baada ya Bruno Fernandes kuwaweka Man-United kifua mbele katika kipindi cha kwanza. Bao la Olise lilitokana na mpira wa ikabu huku la Fernandes likitokana na ushirikiano mkubwa kati yake na Christian Eriksen.

Ushindi kwa Man-United ungalikuwa wao wa 10 mfululizo na ungaliwawezesha kuendeleza presha kwa mabingwa watetezi Manchester City na Arsenal wanaoselelea kileleni mwa jedwali kadri wanavyowania taji la kwanza la EPL tangu 2012-13.

Kufikia sasa, Man-United watakaokuwa wageni wa Arsenal ugani Emirates mnamo Januari 22, 2022, wanakamata nafasi ya tatu jedwalini kwa alama 39 sawa na Man-City ambao wataalika Tottenham Hotspur ugani Etihad mnamo Januari 19, 2022. Arsenal wamejizolea alama 47, tisa zaidi kuliko Newcastle United wanaofunga mduara wa nne-bora.

Matokeo dhidi ya Man-United yalikomesha rekodi duni ya Palace ya kupoteza mechi tatu mfululizo katika mashindano yote. Chini ya kocha Patrick Vieira, Palace kwa sasa wanakamata nafasi ya 12 kwa alama 23. Hata hivyo, ni pengo la pointi nane pekee ndilo linatamalaki kati yao na West Ham United, Everton na Southampton wanaoshikilia nafasi tatu za mwisho.

Palace wangalifunga mabao zaidi kupitia kwa Odsonne Edouard ila kipa David de Gea akajituma maradufu. Man-United walimlalamikia pakubwa refa Robert Jones kuwanyima mkwaju wa penalti baada ya kiungo mvamizi Scott McTominay kukabiliwa visivyo na Chris Richards ndani ya kijisanduku.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Matokeo ya KCSE 2022 yatangazwa rasmi

Kerich akamata nafasi ya pili Doha Marathon, Kipchirchir na...

T L