• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 12:18 PM
Marefarii Thika kupewa mafunzo

Marefarii Thika kupewa mafunzo

Na LAWRENCE ONGARO

MAREFARII wapatao 100 walikongamana katika  uwanja wa Thika Stadium,  ili kutathmini utendaji kazi wao.

Katibu wa FKF tawi la Kati, Paul Gathirwa, alisema timu nyingi zimetoa malalamiko kuhusu uamuzi mbaya kutoka kwa marefa hao uwanjani.

Baadhi ya maswala muhimu yaliyojadiliwa ni kufanya uamuzi wa haki kwa kila klabu, huku kila refarii akishauriwa kujiamini.

Ilidaiwa marefarii wengine hufuata hisia za mashabiki jambo lililokosolewa sana na washika dao wa soka kutoka kaunti ya Kiambu.

Kulingana na katibu huyo iliafikiwa kuwa marefarii watakuwa wakihudhuria kozi fupi za kuwapa mwelekeo kuhusu maswala ya urefarii.

Ilipendekezwa pia kuwa waamuzi hao watalazimika kufika uwanjani masaa mawili mapema kabla ya mechi yeyote kung’oa nanga ili kujuana na makocha wa pande zote mbili za timu na pia kuelewa shida wanazopitia.

Marefarii pia walihimizwa kujiweka timamu kiafya ili kuwa imara wakati wa kuchezesha mechi uwanjani.

Ilipitishwa kuwa marefarii wazembe watachukuliwa hatua ya kinidhamu  huku wakishauriwa kutopendelea timu yoyote.

ilipendekezwa kuwa wakufunzi wenye ujuzi katika kiwango cha FIFA ndio watapewa nafasi ya kuwanoa marefarii wengine.

Marefarii walishauriwa kuwa na uhusiano mwema na wakufunzi na wachezaji wa klabu tofauti.

“Mikutano ya kila mara yatakuwa yakiendelea ili kuelewa matatizo yanayopatikana viwanjani. Hiyo ni muhimu kwa sababu italeta uhusiano mwema katika sekta ya michezo,” alisema Gathirwa.

Marefarii walihimizwa kutafuta uhusiano mwema na wadau wengine katika maeneo tofauti ili kupata mwongozo mwafaka katika fani ya michezo.

  • Tags

You can share this post!

Zetech yatawazwa bingwa wa karate

Liverpool mabingwa wa Carabao Cup

T L