• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Mashindano ya riadha kanda ya Kati yatia fora licha ya mvua

Mashindano ya riadha kanda ya Kati yatia fora licha ya mvua

Na LAWRENCE ONGARO

FAINALI za riadha kwa shule za upili kanda ya Kati zimetia fora katika Shule ya Upili ya M-Pesa Foundation, Thika, licha ya mvua kunyesha, huku wanafunzi kutoka kaunti za Nyandarua, Kiambu, Nyeri na Murang’a wakionyesha ubingwa wao katika michezo hiyo.

Katika mbio za mita 10,000 kwa wavulana, William Kimosop wa Nyandarua alikuwa wa kwanza na kukamilisha kwa muda wa 31:00.0. Calvin  Muthii alikuwa wa pili kwa kutumia muda wa dakika 31:01.0.

Katika kitengo cha mbio za mita 5,000 upande wa wavulana, Julius Leteile (Nyandarua) amemaliza kwa muda wa dakika 13:06.2 naye David Ndichu (Nyandarua) akasajili muda wa 13:09.3.

Katika mita 400 Milton Saini (Murang’a) aliibuka bingwa kwa kutumia muda wa dakika 01:01.2 naye Benjamin Siteiye (Kiambu) akawa wa pili kwa muda 01:01.6.

Katika matembezi ya wasichana mita 5,000 Doris Githae (Nyandarua) amesajili muda wa 28:45.4 akifuatwa na Mercyline Wanjala (Kiambu) 30:06.1.

Katika mbio za mita 5,000 wasichana Marriet Wanjiku (Nyandarua) ameongoza kwa kutumia muda wa 17:20.9 naye Miriam Wangui (Nyandarua) akamfuata kwa muda wa 18:08.5.

Kuruka viunzi kwa wasichana Beatrice kaniva (Kirinyaga) 01:12.1. Lydia Wawira (Nyeri) 01:14.7.

Kurusha jiwe kwa wasichana Delphine Ngesa  (Kiambu) 9:78. Esther Wangari (Kiambu) 9:22.

Kurusha kijisahani (discuss) kwa wasichana Nancy Wairimu (Kirinyaga) 22:11. Pauline Wamuyu (Nyeri) 21:28.

Katibu wa michezo ya shule kanda ya Kati, Virginia Murage, amesema mvua iliyumbisha tu juhudi za wanariadha waliyoshiriki na wala haikuzima juhudi zao.

Alisema kila mchezo, kwa maana ya kategoria, utawakilishwa na wanariadha wawili ambao ni nambari moja na mbili.

Wanariadha wanaoshiriki mbio katika kanda ya Kati. PICHA | LAWRENCE ONGARO
  • Tags

You can share this post!

Paka ajumuika na waumini kwa swala ya Tarawehi

Handiboli: Handege yalipua Mang’u High

T L