• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 5:50 AM
Mchezaji wa zamani wa Gor Mahia kuuza basi la klabu ajilipe mshahara

Mchezaji wa zamani wa Gor Mahia kuuza basi la klabu ajilipe mshahara

NA SAMMY WAWERU

MCHEZAJI wa zamani wa Gor Mahia Wellington Ochieng amepata idhini ya mahakama kuuza basi la klabu hiyo kujilipa malimbikizo ya mshahara wake.

Bw Ochieng, 27, aliwasilisha kesi katika Mahakama ya Milimani, kutwaa basi la timu hiyo aliuze ili ajilipe deni la mrundiko wa mishahara anaoidai.

Baada ya korti kusikiliza upande wa mlalamishi, ilitoa maamuzi ikiruhusu mwanasoka huyo anadi basi la klabu ya Gor.

Alichezea timu hiyo kati ya 2016 na 2018, kwa sasa akiidai zaidi kima cha Sh1 milioni.

“Chini ya amri kutoka Mahakama ya Milimani, tutauza gari lililotajwa hapa na lililotwaliwa na Leakey’s storage Limited, mnamo Machi 15, 2023 saa nne na nusu asubuhi katika afisi zetu,” linasema tangazo la kunadi la Vintage Auctioneers lililochapishwa kwenye gazeti moja nchini.

Tangazo hilo pia limeandamanishwa na nambari ya kesi, ambayo ni CMCE364 of 2022 – Milimani, Wellington Ochieng Omondi-VS-Gor Mahia Football Club.

Basi la timu hiyo ambalo litanadiwa ni Isuzu KBP 040V.

Kutwaliwa kwa gari hilo kumesababisha Gor Mahia kuhangaika, hasa kusafirisha wachezaji wake kufanya mazoezi na kushiriki mechi.

Timu hiyo aidha inakabiliwa na changamoto kifedha, ikiendelea kudaiwa na wachezaji na watoaji huduma.

  • Tags

You can share this post!

GWIJI WA WIKI: Mwanahabari Selly ‘Kadot’ Amutabi

Adhabu kali kutolewa kwa mashoga Uganda

T L