• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 5:17 PM
Mchezaji wa zamani wa Simba, Gor kunoa Meru Bombers

Mchezaji wa zamani wa Simba, Gor kunoa Meru Bombers

Na JOHN KIMWERE

MCHEZAJI wa zamani wa Gor Mahia FC, Moses ‘Dube’ Odhiambo ameteuliwa kocha mkuu wa Meru Mutindwa Bombers ya Ligi ya Taifa Daraja la Pili.

”Tuna furaha tele kutangaza kuwa Dube atakuwa kocha wa Meru Bombers ambapo ni jambo nzuri kuona mchezaji aliyeanza kushiriki soka katika Kaunti ya Meru amerejea nyumbani,” taarifa ya klabu hiyo imesema.

Kiungo huyo ana tajriba ya muda mrefu kwa kuzingatia anajivuia kutwaa taji la Ligi Kuu nchini mara moja na mataji mawili ya FKF Cup alipokuwa nahodha wa Gor Mahia FC.

Aidha anajivunia kushinda Ligi Kuu nchini Tanzania akichezea Simba FC pia akichezea Moro United nchini humo walimaliza nafasi ya pili mara mbili kwenye soka la ubingwa wa Afrika Masharika na Kati.

Kadhalika anajivunia kushiriki soka la kulipwa nchini Rwanda akisakatia APR bila kuweka katika kaburi la sahau kuwa alichezea Kenya All Stars dhidi ya klabu ya Hull City kwenye patashika ya kuwania taji la SportPesa.

Katika taarifa iliyotumwa kwenye tovuti ya klabu hiyo viongozi wake wanasema wana furaha tele kufuatia ujio wa kocha huyo atakayenoa makali ya wachezaji chipukizi wanaohitaji kocha mwenye uzoefu wa muda mrefu.

Serikali ya Kaunti ya Meru tayari imeruhusu klabu hiyo kutumia uwanja wa Kinoru Stadium kuchezea mechi za nyumbani

  • Tags

You can share this post!

Uhuru achomoa minofu kuzolea Raila kura urais

Barcelona waafikiana na Bayern kuhusu uhamisho wa Robert...

T L