• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 5:06 PM
Mechi za CECAFA zaanza bila Kenya

Mechi za CECAFA zaanza bila Kenya

NA JOHN ASHIHUNDU

KENYA ni miongoni mwa mataifa ya CEACAFA yatakayokosa kushiriki katika michuano ya soka ya wasiozidi umri wa miaka 15.

Timu ya Kenya ilikuwa imejumuishwa katika mashindano hayo yatakayoanza kesho Jumamosi nchini Uganda katika kituo cha kunoa vipaji cha FUFA mjini Njeru kati ya Novemba 4 na Novemba 16.

“Badala ya kwenda Uganda, tumeonelea tuendelee kunoa vijana wetu kwa mashindano ya CAF (Zonal Pan African School Games) yatakayofanyika nchini kati ya Disemba 10 na Disemba 15th, ambapo tutawakilishwa na timu tatu kati ya umri wa miaka 13 na 15”, Afisa Mkuu wa FKF, Barry Otieno alisema.

“Hii ndio sababu iliyotufanya tujitenge na michuano ya CACAFA ili tujiandae kwa ile ya CAF,” aliongeza.

Akithibitisha habari hizo, Mkurugenzi Mkuu wa CECAFA, Auka Gacheo alisema tayari waandalizi wa mechi za Njeru wamefanya droo bila kujumuisha Kenya, Sudan, Burundi na Eritrea. Timu zitakazoshiriki ni Uganda, Ethiopia, Djibouti, South Sudan, Tanzania, Zanzibar, Somalia na Rwanda.

Gacheo alisema mashindano hayo ya wiki mbili yanatumika kuandaa vijana wa mataifa hayo kwa michuano ijayo ya AFCON kwa wasiozidi umri wa miaka 17 itakayofanyika mwaka ujao chini ya udhamini wa Total Africa.

Mashindano ya wasiozidi umri wa miaka 15 yalifanyika kwa mara ya mwisho mjini Asmara nchini Eritrea ambapo Uganda walitwaa ubingwa baada ya kuilaza Kenya 4-0 fainalini.

Lakini hayakufanyika kwa miaka mitatu iliyofuata kutokana na sababu mbali mbali, ukiwemo uggonjwa wa Korona uliovuruga shughuli nyingi za michezo kote duniani.

Kulingana na Gacheo, wenyeji Uganda wamepangiwa katika Kundi A linalojumuisha pia timu za Ethiopia, Djibouti pamoja South Sudan, wakati Kundi B likiwa na Tanzania, Zanzibar, Somalia pamoja na Rwanda.

Mechi ya ufunguzi kesho itakuwa kati ya Ethiopia na Sudan Kusini kabla ya wenyeji Uganda kuingia kuchafuana na Djibouti.

Tanzania itafungua mechi zake za Kundi B dhidi ya Somalia Jumapili, kabla ya Zanzibar kupepetana na Rwanda baadaye siku hiyo.

Aakizungmza kuhusu mechi yao ya utangulizi, kocha wa kikosi cha Uganda Hamuza Lutalo alisema vijana wake wamejiandaa vyema kwa pambano hilo, huku wakilenga kiuhifadhi ubingwa.

“Bilas haka, upinzani utakuwa mkali, lakini tumejiandaa kukabiliana vilivyo na upinzani wowote,” alisema Lutalo.

  • Tags

You can share this post!

Huyu Defoe hapoi, anaye Alisha lakini bado anachovya mzinga...

Rais Ruto awashauri maafisa wa KRA wawe na utu kwa walipaji...

T L