• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 8:50 AM
Mkenya Karan Patel aibuka mshindi wa Rwanda Mountain Gorilla Rally

Mkenya Karan Patel aibuka mshindi wa Rwanda Mountain Gorilla Rally

NA GEOFFREY ANENE

DEREVA Mkenya Karan Patel akishirikiana na Tauseef Khan aliibuka mshindi wa duru ya Mbio za Magari za Afrika (ARC) ya Rwanda Muntain Gorilla Rally nchini Rwanda, Jumapili.

Akipaisha gari la Ford Fiesta R5, Karan alikamilisha mbio hizo za siku tatu za kilomita 195.36 kwa saa 1:19:40.3.

Alifuatwa kwa karibu na Mzambia Leroy Gomes/Urshlla Gomes aliyepaisha Ford Fiesta R5 (1:19:53.5), Mkenya Hamza Anwar/Adnan Din wa Ford Fiesta R3 (1:21:21.8), Mganda Jas Mangat/Joseph Kamyai (Mitsubishi Lancer EVO, 1:22:07.4) na Wakenya Jeremiah Wahome/Victor Okundi (Ford Fiesta R3, 1:22:30.0) na McRae Kimathi/Mwangi Kioni (Ford Fiesta R3, 1:23:22:3) katika nafasi sita za kwanza.

Mwanadada Mkenya Maxine Wahome na mwelekezi wake Murage Waigwa katika Ford Fiesta R3 walikamata nafasi ya tisa kwenye duru hiyo ya tano baada ya duru ya Bandama (Ivory Coast), Equator (Kenya), Pearl (Uganda) na Atlantic (Tanzania).

Zaidi ya madereva 20 walianza duru ya Rwanda, lakini ni 14 pekee walikamilisha baada ya wengine kujiuzulu kutokana na matatizo mbalimbali.

Leroy anaongoza jedwali kwa pointi 123 akifuatiwa Karan (100). Karan amechelewesha Leroy kutawazwa bingwa mpya wa Afrika na kufufua matumaini yake mwenyewe. Duru ya Zambia itafunga msimu hapo Oktoba 21-23. 

  • Tags

You can share this post!

Barasa aamrisha idara ya afya idhibiti ebola

Gachagua apingwa kuhusu kauli ya misitu

T L