• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Mkenya-Mserbia Odada ajiunga na Philadelphia Union nchini Amerika kwa Sh24 milioni

Mkenya-Mserbia Odada ajiunga na Philadelphia Union nchini Amerika kwa Sh24 milioni

Na GEOFFREY ANENE

KIUNGO wa mataifa ya Kenya na Serbia, Richard Odada amejiunga na Philadelphia Union inayoshiriki Ligi Kuu ya Amerika na Canada (MLS).

Odada, ambaye amekuwa na miamba wa Serbia, Red Star Belgrade, tangu mwaka 2019, ameelekea Amerika kwa kandarasi ya miaka miwili.

Red Star Belgrade, ambayo ilimpeleka Odada katika klabu za Graficar na Metalac apate ujuzi, aliuzia Philadelphia mchezaji huyo kwa Sh24,166,717 mnamo Agosti 2.

Habari za kiungo huyo mkabaji kutua MLS zilithibitishwa na mkurugenzi wa michezo wa Philadelphia Union Ernst Tanner aliyemsifu Odada kama mchezaji anayeweza kufanya majukumu ya safu ya kati na pia beki wa kati.

“Ana urefu mzuri, kasi na nguvu za kimwili, vitu ambavyo tulikuwa tukitafuta. Tunalenga kumjumuisha kikosini mwaka huu na kuendelea kupalilia talanta yake kwa siku za usoni,” alisema afisa huyo.

Odada aliyetokea timu ya chipukizi ya AFC Leopards, amekuwa nchini Serbia tangu 2017. Aliomba uraia wa Serbia mwaka 2020 baada ya kuishi nchini humo miaka mitatu mfululizo. Alichezea Metalac mara 27 msimu uliopita.

Odada, ambaye alizaliwa Novemba 25 mwaka 2000 jijini Nairobi, anaungana kwenye MLS na kiungo mkabaji Mkenya Victor Wanyama anayechezea CF Montreal.

  • Tags

You can share this post!

Serikali haitafunga mawasiliano ya intaneti – Mucheru

Nyong’o akemea Amerika kwa kubashiri fujo Kisumu

T L