• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Mombasa Elite yailaza Coastal Heroes 1-0 ligi ya NSL

Mombasa Elite yailaza Coastal Heroes 1-0 ligi ya NSL

Na ABDULRAHMAN SHERIFF

MAKOCHA wa timu za Mombasa Elite na Coastal Heroes FC wamekuwa na maoni yaliyofanana juu ya ubora wa wachezaji wao baada ya kukaa bila ya kucheza kwa kipindi cha zaidi ya wiki tatu mechi zao za Ligi ya Kitaifa ya Supa (NSL).

Kocha wa Mombasa Elite FC Mohamed Ahmed almaarufu Mohaa na mwenzake wa Coastal Heroes Mohamed Hussein Madaga, wamesema kuwa kutokana na ligi hiyo kusimama kwa kipindi kirefu, wachezaji wao hawajakuwa na ubora wao wa kawaida.

“Wachezaji wakikosa kucheza mechi kwa muda, hupoteza uchezaji wao wa kawaida. Kucheza mechi kunawasaidia wachezaji kuongeza ubora wao na hivyo kutokana na ligi kusimama, tuko katika kufanyia kazi kurudisha ubora wa wanasoka wetu,” amesema Mohaa.

Alidokeza kuwa baada ya kipindi cha kwanza cha mechi yao na mahasimu wao hao wa Coastal Heroes kuwa sare, alibadilisha mchezo na wachezaji wake wakafuata maagizo na kufanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0; bao lilofungwa dakika ya 71.

Madaga anasema huwezi kuwalaumu wachezaji kwani walijikaza na kucheza mchezo mzuri, lakini bado hawakuwa katika viwango vyao vya kawaida kwa sababu kwa kipindi kirefu cha kutocheza.

“Tulivunja mazoezi mazoezi na ni siku ya Jumatano ya wiki hii ndipo tumewarudisha wachezaji kiwanjani kwa mazoezi na hivyo, matokeo hayo ni ya kawaida kutokea hasa kwa mechi zozote za debi,” akasema mkufunzi huyo wa Heroes.

You can share this post!

Wakenya Nancy Cherono, Jelagat wavuna vinono Valencia...

Onyango atawazwa bingwa wa ndondi

T L