• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 9:50 AM
Onyango atawazwa bingwa wa ndondi

Onyango atawazwa bingwa wa ndondi

Na CHARLES ONGADI

BONDIA George Onyango alimshinda Fred Nyakesha kwa wingi wa alama na kutawazwa bingwa wa taifa katika uzito wa Lightwelter kwenye ukumbi wa Charter, Nairobi, Jumamosi.

Pigano hilo la kuvutia lilihudhuriwa na mwenyekiti na Shirikisho la Ndondi la kulipwa nchini ( KPBC) Reuben Ndolo na viongozi wengine wa Ndondi Nchini akiwemo katibu wa KPBC Julius Odhiambo.

Katika pigano hilo mabondia hawa wawili walipokezana makonde mazito katika raundi zote kumi kabla ya waamuzi kumpatia Onyango ushindi kwa wingi wa alama.Aidha, kulikuwa na mapigano mengine matano yasiyo ya kuwania taji.

Nick ‘ Kanyankole ‘ Otieno alimshinda Joshua Osotsi kwa wingi wa alama katika pigano la uzito wa Super bantam la raundi nane.Otieno ambaye amewahi kuwa katika timu ya taifa ‘ Hit Squad ‘ miaka ya nyuma kabla ya kujiunga na masumbwi ya malipo alidhihirisha kwamba angali moto wa kuotea mbali ulingoni.

Katika pigano lengine,Ken Opiyo alishindwa kujimudu mbele ya Dan Oluoch katika pigano la uzito wa Super welter raundi ya nane.Katika pigano la uzito wa Super bantam, Albert Kimaru alimshinda Calvin Okello kwa wingi wa alama katika pigano la raundi nane.

Naye Denzel Onyango alimkung’uta Kenedy Omondi kwa wingi wa alama katika uzito wa Middle.Hata hivyo, pigano la pekee la akina dada kati Consolata Musanga na Susan Andeso lilikosa kumalizika kama ilivyopangwa baada Musanga kumzidia Andeso katika raundi ya tatu na kupeleka refa kusimamisha pigano hilo.

You can share this post!

Mombasa Elite yailaza Coastal Heroes 1-0 ligi ya NSL

Chelsea yazidisha ukatili

T L