• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 2:00 PM
Mwanariadha Wambui ala marufuku kwa matumizi ya pufya

Mwanariadha Wambui ala marufuku kwa matumizi ya pufya

Na GEOFFREY ANENE

BINGWA wa mbio za mita 800 kwenye Riadha za Dunia za chipukizi wasiozidi umri wa miaka 18 mwaka 2017 na Afrika kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 mwaka 2019 Jackline Wambui atameza mate tu wengine wakitafuta ufanisi baada ya kupigwa marufuku miaka miwili.

Wambui anayejivunia muda bora wa kukamilisha mbio za kuzunguka uwanja mara mbili wa dakika 1:58.79, hajaonekana mashindanoni tangu ajitose katika 5,000m mwezi Machi 2022.

Ameshiriki pia 1,500m, akiandikisha 4:19.48. Wambui alisherehekea kufikisha umri wa miaka 23 hapo Februari 8.

“Mahakama ya kesi za michezo (SDT) imepiga marufuku Jackline Wambui kwa kipindi cha miaka miwili. Hataweza kushiriki mashindano kutoka Desemba 20, 2021. Mwanariadha huyo alishtakiwa na kosa la kutumia dawa za kusisimua misuli za aina ya Norandrosterone,” SDT ilisema katika hukumu yake hapo Februari 15. Alikuwa katika kikosi cha Kenya cha Riadha za Dunia 2019, lakini akaondolewa kwa sababu ya kutotimiza masharti ya kupimwa dawa za kusisimua misuli mara tatu kabla ya mashindano.

Zaidi ya Wakenya 30, wengi wao wanariadha, wanatumikia marufuku kwa matumizi ya pufya.

  • Tags

You can share this post!

Chitembwe afika Mahakama ya Juu akitaka imrudishe kazini

Ruto acheza pata potea ya kiuchumi

T L