• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 12:38 PM
Neymar sasa kuchezea PSG hadi 2025

Neymar sasa kuchezea PSG hadi 2025

Na MASHIRIKA

MSHAMBULIAJI matata raia wa Brazil, Neymar Jr, 29, ametia saini mkataba mpya utakaomdumisha kambini mwa Paris Saint-Germain (PSG) ya Ligi Kuu ya Ufaransa hadi Juni 30, 2025.

Akitia saini kandarasi hiyo, Neymar alikiri kwamba “furaha” ni sababu kuu iliyochochea maamuzi yake hayo.

Neymar aliingia katika sajili rasmi ya PSG mnamo 2017 kwa kima cha Sh26 bilioni kutoka Barcelona. Uhamisho huo ulimfanya kuwa sogora ghali zaidi duniani. Hadi aliporefusha mkataba wake jijini Paris, fowadi huyo alikuwa akihusishwa na uwezekano mkubwa wa kubanduka kambini mwa PSG na kurejea Barcelona.

“PSG wamenipa jukwaa zuri la kua zaidi kama mtu, binadamu na mchezaji,” akasema Neymar aliyekuwa katika mwaka wake wa mwisho kwenye kandarasi yake ya awali ya miaka mitano na PSG.

Tangu ajiunge na PSG, Neymar amefunga jumla ya mabao 85 na kuchangia mengine 51 kutokana na mechi 112.

Hata hivyo, amekuwa na kipindi kigumu kudumisha uhusiano mwema kati yake na mashabiki wa kikosi hicho tangu afichue azma ya kurejea Barcelona mnamo 2019.

PSG ambao kwa sasa wanafukuzia taji lao la nne mfululizo katika Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1), wanashikilia nafasi ya pili kwenye msimamo wa jedwali kwa alama 75, nne nyuma ya viongozi Lille ambao wametandaza mechi moja zaidi.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Papa Francis aunga kuondolewa kwa ulinzi wa hakimiliki za...

Alexis Sanchez afunga mabao mawili na kusaidia mabingwa...