• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 9:50 AM
Niliyoyachukulia ni mambo madogo tu yamenivunia heshima ambayo sikutarajia – Kipchoge

Niliyoyachukulia ni mambo madogo tu yamenivunia heshima ambayo sikutarajia – Kipchoge

Na GEOFFREY ANENE

BINGWA mara mbili wa mbio za marathon za Olimpiki, Eliud Kipchoge amesema kuwa ni heshima kubwa kupokea Shahada ya Heshima ya Udaktari ya michango yake ya uhisani kwa Jamii (Honoris Causa) kutoka kwa Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT).

“Najivunia na kunyenyekea kupokea kutambuliwa kwa kile nachukulia kuwa juhudi ndogo za kuendeleza utu na maendeleo katika jamii kupitia kwa wakfu wa Eliud Kipchoge,” akatanguliza Kipchoge kwenye mtandao wa X mnamo Jumamosi.

Kupokea tuzo hiyo, akasema Kipchoge, ni heshima ya kibinafsi na inachochea ari ya kujitolea kusaidia mfumo wa elimu nchini Kenya na juhudi za kulinda mazingira hapa nyumbani na ughaibuni.

“Nashukuru seneti na baraza la Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta cha Kilimo na Teknolojia kwa kunipa utambuzi huo. Tuchangieni sote katika kufanya dunia kuwa mahali pazuri, tuinue umuhimu wa elimu bora na kulinda mazingira,” akasema mshikilizi wa zamani wa rekodi ya dunia ya saa 2:01:09 ambayo Mkenya mwenzake Kelvin Kiptum alivunja akishinda Chicago Marathon kwa 2:00:35 mwezi Oktoba 2023.

Si shahada ya kwanza ya heshima Kipchoge amepata baada ya pia Chuo Kikuu cha Laikipia kumpa digrii ya masuala ya Sayansi mwezi Desemba mwaka 2019.

  • Tags

You can share this post!

Serikali kupendekeza sheria ya kudhibiti soko la hewa ukaa...

Wauzaji pombe ‘mwitu’ kuona cha mtema kuni

T L