• Nairobi
  • Last Updated December 5th, 2023 8:55 PM
Nyati FC pabaya katika Ligi ya NERL

Nyati FC pabaya katika Ligi ya NERL

NA JOHN KIMWERE
KOCHA  Michael Wanjohi  wa Nyati FC amesema wamejikuta pabaya kwenye kampeni za mechi za Zoni C Ligi ya Kanda ya Nairobi Mashariki (NERL) msimu huu.
Amedokeza kuwa wamejikuta kaika mduara wa kushushwa ngazi baada ya kuandikisha matokeo mbovu kwenye mechi za mwisho. Kocha huyo amefunguka hayo baada ya kushinda mechi moja kwa mabao 3-2 dhidi ya Kamongo FC. Hata hivyo ilipoteza patashika moja ilipocharazwa mabao 2-0 na Maafande wa Gunners.
Nyati FC ilipata ushindi huo kupitia Joseph Bosco, Rodgers Mbasu na Elvis Omolet waliocheka na wavu mara moja kila mmoja. Naye Omara Boraafya alifungia Gunners FC mabao yote.
”Sasa tunasubiria uamuzi wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) kufahamu tumesalia upande gani kwa sasa bado hawajatoa ripoti kamili ni timu ngapi zinashushwa ngazi,” kocha wa Nyati alisema.
Aliongeza kuwa wanashikilia nafasi ya 11 na huenda wakaponea. Hata hivyo anashikilia kuwa walipania kumaliza kati ya nafasi nane bora lakini waliteleza kwenye mechi za mwisho.
Kwenye matokeo hayo, Creative Hands ilipigwa bao 1-0 na Burhan, A-1000 Sportifnf ilicharaza Hakati Sportiff mabao 2-0 huku Shalom FC iikizoa ushindi kama huo dhidi ya Tena City FC. Licha ya Creative Hands kupoteza mechi ya mwisho imemaliza kileleni kwa 71, 15 mbele ya Jericho Allstars.
  • Tags

You can share this post!

Utalii Lamu wayumbishwa na Al-Shabaab

Wakenya sasa kukamuliwa

T L