• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 6:55 AM
Okutoyi ateremka viwango bora bora tenis

Okutoyi ateremka viwango bora bora tenis

Na GEOFFREY ANENE

Angella Okutoyi ameshuka nafasi mbili kwenye viwango bora vya Shirikisho la Kimataifa la Tenisi (ITF) vilivyotangazwa Aprili 12 baada ya kusikitisha mashindanoni juma lililopita mjini Sfax, Tunisia.

Okutoyi sasa anakamata nambari 155 duniani.

Akiorodheshwa 153 duniani mnamo Aprili 5 na wa kwanza kabla ya mashindano ya daraja ya tano (J5) ya Sfax, Okutoyi,17, aliduwazwa na Amina Zeghlouli,13, kwa mbili kavu za 6-1, 6-3 katika mechi yake ya kwanza. Mmoroko huyo, ambaye aliingia J5 Sfax akishikilia nambari 1962 duniani, ameruka juu nafasi 533 na sasa anapatikana 1429 duniani baada ya kufika nusu-fainali ya mashindano hayo yaliyoandaliwa Aprili 6-11.

Okutoyi ameratibiwa kurejea ulingoni kwa mashindano ya daraja ya tatu (J3) yatakayofanyika Megrine nchini Tunisia mnamo Aprili 13-18.

Okutoyi, ambaye alitawala mashindano mawili ya daraja ya nne (J4) jijini Nairobi mwezi Januari na kuruka kutoka 186 duniani hadi 127, hakuwa Mkenya wa pekee kupoteza kwenye viwango hivyo vipya. Pacha wake Roselida Asumwa ameteremka nafasi nane hadi nambari 1257. Alicia Owegi amepaa nafasi 29 na kutulia katika nafasi ya 1504. Shania Gadhia na Cynthia Wanjala wameshuka nafasi sita na kukamata kwa pamoja nambari 2043. Shakira Varese yuko chini nafasi nane. Anashikilia nambari 2293.

  • Tags

You can share this post!

Kocha Ouma apigwa kalamu, FKF yaajiri More kung’oa...

Ielewe teknolojia ya 5G iliyozinduliwa na Safaricom na...