• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:55 AM
Okutoyi tayari kutafuta ufanisi katika mechi ya mchezaji mmoja kila upande US Open

Okutoyi tayari kutafuta ufanisi katika mechi ya mchezaji mmoja kila upande US Open

Na GEOFFREY ANENE

NYOTA Angella Okutoyi yuko tayari kwa mashindano ya tenisi ya chipukizi ya J1 Repentigny na US Open.

Hata hivyo, Okutoyi amekiri analenga kuimarisha mchezo wake katika kitengo cha mchezaji mmoja kila upande ili kupata ufanisi zaidi baada ya kushinda michuano tatu kati ya 12 iliyopita.

Ameeleza Taifa Leo kuwa amejiandaa vyema kwa mashindano ya J1 Repentigny na US Open yatakayofanyika nchini Canada na Amerika mnamo Agosti 28 hadi Septemba 3 nayo US Open ni Septemba 4-10 mtawalia.

“Nimejitayarisha vyema na ninatumai kusafiri Jumatatu. Nataka kucheza vizuri. Nataka kutumia Repentigny kupata motisha ya kujiamini kwa sababu katika mashindano kadha sasa nimekuwa nikifanya vyema katika kitengo cha wachezaji wawili kila upande, lakini si katika kitengo cha mchezaji mmoja kila upande. Nataka kupata kujiamini tena katika kitengo cha mchezaji mmoja kila upande kupitia shindano la Repentigny kabla ya kuelekea US Open,” alisema Okutoyi ambaye juma hili amepewa uanachama wa chipukizi katika klabu ya michezo ya kibinafsi ya Nairobi Club hadi atakapofikisha umri wa miaka 25 na pia na klabu ya Karen Country Club kwa kipindi cha miaka mitatu.

Bingwa huyo wa zamani wa Kenya Open 2018 na Afrika kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18 mwaka 2021 pia alishukuru wadhamini ambao wamekuwa wakijitokeza kumpiga jeki.

Mbali na uanachama kutoka Nairobi Club na Karen Country Club, Okutoyi pia alishinda tuzo ya mwanamichezo bora wa Julai wa tuzo ya LG/SJAK akipewa runinga ya LG Nanocell inayogharimu Sh120,000 madukani.

  • Tags

You can share this post!

NYOTA WA WIKI: Wilfried Zaha

VITUKO: Neuer ajiandaa kuishi na Anika raha mustarehe

T L