• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 5:55 AM
Omanyala azoa taji la mbio za mita 100 Jumuiya ya Madola

Omanyala azoa taji la mbio za mita 100 Jumuiya ya Madola

Na GEOFFREY ANENE

BINGWA wa Afrika mbio za mita 100 Ferdinand Omanyala sasa pia ni mfalme wa michezo ya Jumuiya ya Madola katika umbali huo baada ya kutifulia wapinzani wake vumbi mjini Birmingham, Uingereza, Jumatano usiku.

Omanyala, ambaye anashikilia rekodi ya Afrika ya sekunde 9.77, alitwaa taji la Jumuiya ya Madola kwa sekunde 10.02.

Kwa mara nyingine, alivua raia wa Afrika Kusini Akani Simbine ubingwa.

Simbine alipoteza taji la Afrika kwa Omanyala mjini Reduit, Mauritius mwezi Juni kabla ya kusalimu amri tena mjini Birmingham.

Omanyala pia alivunja rekodi ya Simbine ya Afrika ya 9.84 mwaka 2021 wakati wa Kip Keino Classic uwanajni Kasarani jijini Nairobi.

Simbine aliridhika na nafasi ya pili mjini Birmingham kwa sekunde 10.13 naye Yupun Abeykon kutoka Sri Lanka akanyakua nishani ya shaba kwa 10.14.

Omanyala, ambaye alikuwa ameahidi taji la Jumuiya ya Madola chini ya sekunde 10, ni Mkenya wa kwanza kushinda dhahabu ya mita 100 kwenye Jumuiya ya Madola tangu Seraphino Antao mwaka 1962.

  • Tags

You can share this post!

Hali ya usalama imeimarishwa Laikipia – Serikali

Watetezi washinikiza Gachagua, viongozi 13 wazuiwe kuwania

T L