• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 1:46 PM
Omanyala, Shelly-Ann Fraser-Pryce tayari kufyatuka kasi ya juu Botswana

Omanyala, Shelly-Ann Fraser-Pryce tayari kufyatuka kasi ya juu Botswana

Na AYUMBA AYODI

BINGWA wa Afrika, Jumuiya ya Madola na Kip Keino Classic mbio za mita 100, Ferdinand Omanyala pamoja na Mjamaica Shelly-Ann Fraser-Pryce wamethibitisha kuwania taji la Botswana Golden Grand Prix hapo Aprili 29.

Mshindi wa Olimpiki mbio za 400m mwaka 2012, Kiran James kutoka Grenada pia ameingia duru hiyo ambayo imejumuishwa katika mashindano ya Continental Tour ya Shirikisho la Riadha Duniani kwa mara ya kwanza.

Ni mojawapo ya duru 14 mwaka 2023 za nyota ya dhahabu. Afrika ina duru mbili pekee za kiwango cha dhahabu. Duru nyingine ni Kip Keino Classic itakayofanyika ugani Kasarani hapo Mei 13.

Fraser-Pryce almaarufu Mommy Rocket, ana mataji 10 ya dunia likiwemo la mwaka jana kutoka jimboni Oregon. Amesema kuwa kwa mara nyingine ataanzia msimu barani Afrika ambapo analenga kuandikisha muda mzuri.

“Nitakuwa nikirejea Afrika, mara hii katika duru ya Botswana. Nasubiri kwa hamu kubwa kufungua msimu wangu barani Afrika,” alisema Fraser-Pryce aliyenyakua taji la Kip Keino Classic la 100m kwa sekunde 10.67 mwaka 2022.

“Kila mtu ajiandae kuniona nikifyatuka kwa hivyo kila mtu atafute tiketi yake na awe tayari katika viti vya mashabiki kushuhudia nikifanya mambo makubwa na kufurahia,” alisema bingwa huyo wa Olimpiki mwaka 2008 na 2012.

Mshikilizi wa rekodi ya Afrika ya 100m (sekunde 9.77) Omanyala ameeleza mashabiki wajiandae kwa muda bora nchini Botswana.

“Naahidi burudani tosha…Nitajaajaa katika uwanja wa kitaifa wa Gaborone,” aliapa Omanyala.

Afisa huyo wa polisi aliduwaza Mwamerika Fred Kerley katika fainali ya Kip Keino Classic akitwaa 9.85 mwezi Mei mwaka 2022. Kerley, ambaye aliridhika na nafasi ya pili kwa 9.92, alinyakua taji la dunia mjini Eugene, Oregon mwezi Julai.

Bingwa wa dunia 2011 na Jumuiya ya Madola 2014, Kirani atakimbia kusini mwa jangwa la Sahara kwa mara ya kwanza kabisa.

TAFSIRI: GEOFFREY ANENE

  • Tags

You can share this post!

Wetang’ula ashauri EALA ipigwe jeki

Kenya U13 yaelekea Uingereza kwa raga za kimataifa za...

T L