• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Platinum yarudisha mkono kwa jamii kwa kukuza talanta za vijana mtaani

Platinum yarudisha mkono kwa jamii kwa kukuza talanta za vijana mtaani

Na PATRICK KILAVUKA

PLATINUM FC inapatikana jijini Nairobi inawazia kushiriki Ligi ya Kanda, Shirikisho la Soka Kenya, Nairobi West mwaka 2023.

Ilikosa kiduchu kufuzu ligi hiyo msimu wa 2020-2021 baada ya kuhitimisha Ligi ya Kaunti FKF, Nairobi West katika nafasi ya tatu.

Inafanyia mazoezi Shule Msingi ya Nairobi kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa jioni baada ya kuchapa kazi, japo michuano ya ligi inapigwa uga wa BP, Kawangware.

Wengi wa wanasoka ni wale ambao wanafanya kazi za afisi na mauzo katika kampuni ya Platinum.

Huo ni mwaka wao wa pili tangu timu hii iasisiwe na inaonyesha uwezo wake kuwa moto kuotewa mbali katika kabumbu.

Inaendeleza safari ya ligi kwa kutoka sare ya 1-1 dhidi ya UoN Olympic uwanjani UoN, wikendi iliyopita, japo kocha wake alisema hakutarajia hayo matokeo kwani timu yake ilikuwa imedhibiti mchezo lakini ikasusua tu katika dakika za mwisho wa kipindi cha pili na utepetevu huo ukaigharimu timu baada ya goli hilo kufutwa.

Vijana wa kikosi cha akiba cha Platinum FC wakitazama kwa makini mchuano wa Ligi ya Kaunti, FKF, Nairobi West ambapo Platinum ilicheza dhidi ya UoN Olympic. PICHA | PATRICK KILAVUKA

Inafadhili na kampuni ya Platinum ambayo inapatikana International Life House mkabala wa Mama Ngina.

Madhumuni ya kustawisha timu hii yalikuwa kurudishia jamii mkono na njia ya kusawazisha mawazo kwa wafanyakazi.

Mbali na timu hii, Platinum imepanuliwa ubavu kwa kustawisha timu nyingine ya mtaani Kawangware iitwayo Sates FC ambayo imesajiliwa katika ligi ya Kauntindogo ya FKF,Nairobi West kukuza talanta za mtaani.

Iko chini ya benchi kocha Richard Simbala na msaidizi wake Charles Kimutai.

Kocha huyo alikiri kwamba mnato wa timu umetokana na wachezaji kuwa na umoja kwani, wanafanya kazi mahali pamoja, wengi wanacheza na moyo wa ari ya kupenda soka na fursa adimu wanasoka hawa hupata baada ya kufanya kazi wanakimbia kujifua kwa kuhudhuria mazoezi.

Changamoto imekuwa kwamba wakati mwengine wachezaji hawapatikani wote mara moja kwenye uwanja kwa sababu ya kikazi.

Platinum FC ya jijini Nairobi. PICHA | PATRICK KILAVUKA

  • Tags

You can share this post!

Middlebrough yadengua Man-United kwenye Kombe la FA kupitia...

VOLIBOLI: Kocha wa Prisons asema wako ngangari kukabili...

T L