• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 3:57 PM
Qatar yaweka rekodi kwa kuandaa Kombe la Dunia katika mazingira mazuri

Qatar yaweka rekodi kwa kuandaa Kombe la Dunia katika mazingira mazuri

NA JOHN ASHIHUNDU

MARA tu walipopewa fursa ya kuandaa Kombe la Dunia mnamo 2010, taifa la Qatar liliweka utaratibu wa kuhakikisha kila kitu kilichohitajika kufanikisha mashindano hayo, kimepatikana kwa wakati unaofaa.

Qatar ilijenga viwanja vipya saba- Al Bayt, Al Thumana, Stadium 974, Ahmed Bin Ali, Education City, Al Janoub na ule wa Khalifa International ambao ulifanyiwa marekebisho.

Baada ya Kombe la Dunia kumalizika, tayari uwanja wa Al Janoub uliokuwa na uwezo wa kubeba mashabiki 40,000 umepunguzwa na kubakia wa kubeba 20,000 utatumika kuandaa michezo mbali mbali pamoja na burudani.

Uwanja mkubwa zaidi kwa vyote ni ule wa Lusail Stadium ambao ulivutia zaidi ya mashabiki 88,000 wakati wa fainali kati ya Argentina na Ufaransa, lakini sasa utaanza kutumika kwa shughuli za kijamii, pia kuna nafasi ya shule, maduka, mikahawa, zahanati, mbali na uandalizi wa michezo mbali mbali.

Mfalme wa taifa hilo, Amir Sheikh Tamin bin Hamad al-Thani, bila shaka ameifanya nchi hiyo kutambuliwa kimataifa kutokana na mchango wake mkubwa katika maandalizi ya kufanikisha mashindano ya Kombe la Dunia yaliyomalizika mwishoni mwa wiki.

You can share this post!

Kombe la Dunia lilikuwa na ufanisi mkubwa

MUME KIGONGO: Mwanamume atunze afya kupata mbegu bora ya...

T L