• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Raha tele mwanariadha Kasyoka akimtunuku baiskeli daktari wa viungo Alex Otieno

Raha tele mwanariadha Kasyoka akimtunuku baiskeli daktari wa viungo Alex Otieno

Na GEOFFREY ANENE

MNYANYUAJI wa zamani wa kimataifa wa Kenya Alex Otieno ameelezea furaha yake baada ya mwanzilishi wa Machakos Great Run Festus Kasyoka Mbuva kumpatia baiskeli ya magurudumu matatu ugani Nyayo.

Otieno aliyewakilisha Kenya katika michezo ya Afrika, Jumuiya ya Madola na Olimpiki ya walemavu, alipewa baiskeli hiyo inayogharimu Sh27,000 kwa sababu ya ukarimu wa kutibu Kasyoka bila malipo miaka iliyopita.

“Nakumbuka Kasyoka alikuja katika chumba changu cha kunyoosha viungo hapa Nyayo miaka iliyoenda akiwa mwanariadha akitatizwa na msuli. Nilimnyoosha na akapata nafuu na kuendelea na utimkaji. Nafurahi sana kuwa amenikumbuka kwa kuniletea baiskeli hii ambayo kwangu naiona kama miguu mipya,” alisema Otieno ambaye baada ya kustaafu kunyanyua uzani aliingilia udaktari wa viungo.

Nyota Paul Tergat, Catherine Ndereba na Douglas Wakiihuri ni baadhi ya wanamichezo waliopata kutibiwa na Otieno.

Kasyoka, ambaye ni kocha wa riadha aliyehitimu na pia mkazi wa Amerika na Machakos, anaamini Otieno anaweza kunufaika zaidi akipata fursa ya kufanya kazi hiyo ya udaktari wa viungo.

Kasyoka, ambaye alihamia Amerika miaka 21 iliyopita akiwa na umri wa miaka 19, anafanya kazi na wanariadha 300 katika eneo la Lowen, Massachussets nchini humo wanaotimka mbio za kati ya mita 800 na marathon. Ugonjwa wa polio ulimfanya Otieno kuwa mlemavu akiwa na umri wa miaka tisa.

  • Tags

You can share this post!

Gachagua, Karua waanika wazi ukwasi wao

CHARLES WASONGA: Uhuru na Mohamud wasuluhishe zogo la mpaka...

T L