• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 6:50 AM
Rais wa Estonia ajiunga na Wakenya kwenye mbio katika msitu wa Karura

Rais wa Estonia ajiunga na Wakenya kwenye mbio katika msitu wa Karura

Na GEOFFREY ANENE

RAIS wa Estonia, Kersti Kaljulaid aliungana na Wakenya kwa mbio za kilomita 10 kwenye msitu wa Karura viungani mwa jiji la Nairobi hapo Septemba 11.

Mbio hizo zilianzishwa na Waziri wa Michezo CS Amina Mohammed akiandamana na Waziri wa Ulinzi Monica Juma.

Pia, mashujaa wa mbio humu nchini wakiwemo bingwa wa marathon duniani mwaka 1987 Douglas Wakiihuri, bingwa mara tatu wa mbio za kilomita 21 duniani Tegla Loroupe na bingwa wa marathon duniani mwaka 2003 na 2007 Catherine Ndereba walishiriki mbio hizo zilizofanyika Jumamosi asubuhi.

Rais Kaljulaid amekuwa nchini Kenya tangu Septemba 9 kwa ziara ya siku tatu.

Rais wa Estonia, Kersti Kaljulaid (mbele kushoto) akishiriki mbio za kilomita 10 kwenye msitu wa Karura, Nairobi, Septemba 11, 2021. Picha/ Hisani

Bi Kaljulaid pia amepata kukutana na Rais Uhuru Kenyatta.

“Tumefanya mazungumzo kuhusu uhusiano wa mataifa haya mawili, ushirikiano wa kiuchumi, vita dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 na majanga ya tabia ya nchi na mazingira. Kuna uwezo mkubwa katika mataifa yetu, wananchi na biashara kushirikiana,” Rais Kaljulaid alisema kupitia mtandao wake wa Twitter.

You can share this post!

Oyoo ajaza nafasi ya nahodha Amonde, Simiyu pia ajumuisha...

UMBEA: Je, wewe ni gusa mara moja au mbio ndefu na hufiki...