• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Red Carpet inataka miaka minne ili kutinga ligi kuu ya FKF PL

Red Carpet inataka miaka minne ili kutinga ligi kuu ya FKF PL

Na JOHN KIMWERE

KLABU ya Red Carpet ni kati ya vikosi vinavyopania kujituma mithili ya mchwa kwenye kampeni za kuwania taji la Nairobi West Regional League (NWRL) msimu mpya.

Kikosi hicho kitashiriki kinyang’anyiro hicho baada ya kumaliza nafasi ya saba kwenye mechi za Kundi B muhula uliyopita. Kocha` wake, Meshack Osero Onchonga anasema kuwa raundi hii hawatakuwa na la ziada bali wamepania kupambana mwanzo mwisho kuhakikisha wameibuka kidedea na kutwaa tiketi ya kufuzu kupandishwa ngazi kushiriki mechi za Ligi ya Taifa Daraja la Pili.

”Kiukweli tumetosha kushiriki mechi za kiwango hicho tunataka kupanda ngazi kucheza michuano ya hadhi ya juu huku tukizidi kukuza talanta za wanasoka wetu,” alisema na kuongeza kuwa endapo Kenya ikajipata njia panda endapo Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) litaipiga marufuku ya kutoshiriki mechi za kimataifa kutokana na ishu ya rais wa FKF, Nick Mwendwa. Katika mpango mzima kocha huyu anasema itakuwa vibaya sana endapo Kenya itapigwa marufuku.

Hakuna mteremko

Hata hivyo kocha huyo anasema anafahamu wazi kuwa kampeni za ngarambe hiyo hazitakuwa mteremko. Amazitaja baadhi ya timu zinazotazamiwa kushushwa ushindani wa kufa kama Melta Kabiria, Kemri FC, South B United, AFC Leopards Youth, Amazon Tigers FC na Makarios 111 FC (Riruta United) kati ya zingine.

Sajili wapya

Klabu hiyo imepoteza huduma za wachezaji wawili, Ken Juma na Eric Kenzo ambayo wamejiunga na timu ya Ogopa Kenya School of Government (KSG).

”Kwetu ni pigo kubwa kukosa huduma za wawili hao lakini tumesaini wengine kwenye juhudi za kujaza nafasi zilizoachwa wazi,” akasema.

Timu hiyo imetwaa huduma za wachezaji wapya akiwamo: Isaac Sawanga, Kevin Kamatsi, Alex Ng’ang’a na Patrick Otiende.”Tunaamini wachezaji hao watachochea wenzao na kufanya kweli kwenye kampeni za kinyang’anyiro cha msimu ujao,” alisema na kuwashauri kuwa itabidi wajitume ili kutimiza azimio lao kufuzu kusonga mbele.

Aidha alisema kuwa wanafahamu hakuna kizuri hupatikana rahisi itawabidi wachezaji wao wajifunge kimbwembwe kufukuzia azma yao kupiga hatua kuhakikisha wamefuzu kushiriki Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka la Kenya (FKF PL) ndani ya miaka ijayo.

Tim Wanyonyi

Klabu hiyo tangia ianzishwe 2007 inajivunia kushinda taji la Tim Wanyo

Wachezaji wa timu ya Red Carpet…Picha/JOHN KIMWERE

nyi Super Cup 2018 ilipolaza Leeds United mabao 4-2 kupitia mikwaju ya penalti baada ya kutoka nguvu sawa goli 1-1. Timu hiyo ilishinda ubingwa huo baada ya kulinyemelea kwa miaka mitatu mfululizo huku ikiweka tumaini kuwa baada ya dhiki ni faraja.

Kocha huyo anadokeza kuwa kwa mara nyingine wamepania kujituma kiume kwenye kampeni za shindano hilo kuhakikisha wanalishinda kwa mara ya pili kwenye mechi za mwaka huu. Huenda mechi za kupigania taji hilo zikazinduliwa mapema wiki ijayo. Tayari mabingwa watetezi, Leads United imeapa kupigana kufa mtu kutetea taji hilo ililoshinda mwaka uliyopita.

Red Carpet inajumuisha wachezaji kama: John Kamau, Mike Katanga, Frank Mmani, Fredrick Owino, Godfrey Odongi, Timothy Murunga, Fidel Ishiaho, Radioti Mudhaji, Daniel Arasa, Dennis Oyato, Stephen Githinji, Geofrey Alma, Eric Shiva, Brian Akinyi, Duke Abuja, Mutia Mutinda na Vincent Agwero.

Kocha huyo anasema kuwa ukosefu wa viwanja vya kutosha huchangia timu nyingi kutopata muda wa kushiriki mazoezi. Mfano uwanja wa Kihumbu-ini Kangemi hutumiwa na timu zaidi ya kumi ambapo nyakati zingine vikosi zingine hukosa nafasi.


Wachezaji wa timu ya Red Carpet…
Picha/JOHN KIMWERE

 

You can share this post!

Fahamu vikosi 13 kati ya 32 ambavyo tayari vimefuzu kwa...

Chinese wakali wamlemea, uigizaji wampa ajira

T L