• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Rising Starlets waendelea kujifua dhidi ya Cameroon kuwinda tiketi ya Kombe la Dunia U-20

Rising Starlets waendelea kujifua dhidi ya Cameroon kuwinda tiketi ya Kombe la Dunia U-20

NA TOTO AREGE

TIMU ya taifa ya soka ya Kenya ya wanawake wasiozidi umri wa miaka 20, Rising Starlets, inaingia siku ya sita sasa kambini, wanapojiandaa kwa mechi dhidi ya Indomitable Lionesses ya Cameroon kusaka tiketi ya Kombe la Dunia 2024.

Katika mechi ya kwanza, Kenya itaanza kampeni yake ugenini Jumamosi na kurejea nyumbani kwa mechi ya marudiano Novemba 17, 2023.

Kulingana na nahodha mpya wa Starlets, Rebecca Kwoba, kazi itaendelea walipoachia dhidi Angola mnamo Oktoba.

Kenya ilipata tiketi ya kuingia raundi ya tatu ya mashindano hayo baada ya kuinyeshea Angola jumla ya mabao 10-1.

“Ushindi wa hivi karibuni dhidi ya Angola ulileta motisha kikosini. Licha ya uzoefu wao, tuko tayari kuimarisha mchezo wetu na kuhakikisha tunapata ushindi mwingine,” alisema Kwoba.

Beki huyo, atachukua nafasi ya nahodha Jane Hato ambaye anafanya mtihani wake Kidato cha Nne (KCSE) ambao ulianza Jumatatu.

Wachezaji Velam Abirwe, Charity Luhavi, na Eunice Nabwoba, wote wa Wiyeta Girls, ndio wachezaji wa pekee ambao hawajaingia kambini.

“Wachezaji wamehamasika na wamejipanga kabisa kutoa matokeo mazuri. Tunajiamini na mashabiki hivi karibuni watatuona tukifuzu kwa Kombe la Dunia,” aliongeza Kwoba.

Kikosi hicho chini ya kocha Beldine Odemba, kina wachezaji 19 wapya kati ya wachezaji 35 walioitwa kambini wiki iliyopita.

  • Tags

You can share this post!

Serikali yakataza vyuo vikuu kuajiri wafanyakazi wa ngazi...

Matumaini teknolojia mpya ya kutibu ugonjwa wa selimundu...

T L