• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 5:36 PM
Sababu ya Aubameyang kukosa mechi ya Gabon dhidi ya Ghana

Sababu ya Aubameyang kukosa mechi ya Gabon dhidi ya Ghana

Na MASHIRIKA

FOWADI wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang alikosa kuunga kikosi kilichotegemewa na Gabon dhidi ya Ghana kwenye mechi ya Kombe la Afrika (AFCON) nchini Cameroon mnamo Ijumaa kutokana na matatizo ya moyo yaliyochangiwa na Covid-19.

Hata hivyo, madaktari wa timu ya taifa ya Gabon wameshikilia kwamba sogora huyo anaendelea kupata nafuu na hayuko katika hatari yoyote.

Aubameyang alipatikana na virusi vya corona pindi alipowasili nchini Cameroon kwa ajili ya fainali za AFCON wiki iliyopita.

Kiungo wa zamani wa Southampton, Mario Lemina ambaye sasa anachezea Nice ya Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) pia ametupwa nje ya kikosi cha Gabon kwa sababu hiyo.

Gabon wanaonolewa na kocha Patrice Neveu, walifungua kampeni zao za Kundi C kwenye AFCON nchini Cameroon kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Comoros mnamo Januari 10, 2022 kabla ya kuambulia sare ya 1-1 dhidi ya Ghana mnamo Januari 14, 2022.

Aubameyang ambaye pia aliwahi kuugua Covid-19 mnamo Agosti 2021, alipokonywa utepe wa unahodha kambini mwa Arsenal mnamo Disemba 2021 kwa sababu ya utovu wa nidhamu.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Manchester City wapiga Chelsea na kujiweka pazuri kuhifadhi...

COVID-19: Mechi ya EPL kati ya Tottenham na Arsenal...

T L