• Nairobi
  • Last Updated December 4th, 2023 6:37 PM
Shabana yasajili sita, wengine wakitarajiwa kuwasili

Shabana yasajili sita, wengine wakitarajiwa kuwasili

NA JOHN ASHIHUNDU

SHABANA FC imesajili wachezaji watano huku ikitarajia kuvutia wengine sita kujaza nafasi za walioondoka kujiunga na timu nyingine.

Akitangaza majina hayo, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Elizaphan Kerama alisema timu hiyo imekuwa ikijinoa dhidi ya timu za daraja la chini, lakini itaanza kujipima nguvu na timu za daraja la juu kuanzia wikendi hii.

Mnamo Jumamosi, kikosi hicho cha kocha Sammy Okoth kimepangiwa kucheza na Migori Youth wanaoshiriki Supa Ligi (NSL), kabla ya kuelekea Nairobi kucheza na Bandari na baadaye Kenya Commercial Bank (KCB).

Kerama alisema mechi hizo za kirafiki zitampa kocha fursa ya kupima viwango vya wachezaji wake kabla ya msimu mpya kuanza rasmi hapo Agosti 26.

“Tumehifadhi wachezaji 19 waliokuwa kikosini msimu uliopita, lakini tutajaza nafasi hizo ili tuwe na wachezaji 30 kulingana na matakwa ya sheria za soka. Kufikia sasa tumepata mshambuliaji Johana Mwita, mlinzi Aloro Ayieko wote kutoka Nzoia Sugar, beki wa kushoto, Hillary Wandera pamoja na kiungo, Mark Okolla aliyesakatia Vihiga United msimu uliopita.

  • Tags

You can share this post!

AFC Leopards kupiga kambi Kakamega kujinoa kwa msimu mpya

Mahakama yatupa ombi la kutaka Wajaluo wajitenge na Kenya

T L