• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Shikanda asema ladha ya ligi iliisha Juni 30

Shikanda asema ladha ya ligi iliisha Juni 30

Na JOHN ASHIHUNDU

MWENYEKITI wa klabu ya AFC Leopards Dan Shikanda amefichua kwamba ladha ya Ligi Kuu ya FKF PL iliisha mara tu Tusker walitawazwa wawakilisha wa Kenya kwenye michuano ya Caf msimu ujao, huku Gor Mahia wakishiriki kwenye Caf Confederation Cup.

Leopards walikuwa miongoni mwa timu zilizokuwa zikipigania nafasi hiyo, lakini Tusker wakaipata baada kuwa uongozini kufikia Juni 30, kama ilivyokuwa imepangwa kufuatia agizo la Caf.

Kufikia wakati mabingwa hao wa zamani wakipewa fursa hiyo ya kuwakilisha Kenya katika michuano hiyo ya Klabu Bingwa barani Afrika, KCB walikuwa katika nafasi ya pili, mbele ya Leopards.

Shikanda alisema hata huenda timu zingine zikaanza kupuuza mechi hizo kwa vile tayari mwakilishi wa Kenya katika mashindano ya bara wamejulikana.

“Hamu ya ligi ilimlaizika Juni 30 wakati Tusker walipokezwa tiketi ya kushiriki michuano ya Klabu Bingwa, na hata sielewi tunachezea nini sasa wakati wawakilishi wamesha tambuliwa.

“Ikiwa tayari wameamua timu itakayoshiriki michuano ya Afrika, timu zingine zinachezea nini?, kwa sababu hata kama timu nyingine itaibuka mshindi kufikia Agosti 22 itafaidika vipi na nafasi hiyo?

“Tunacheza ligi kupigania tiketi ya kuwakilisha taifa katika mashindano ya bara, wala sio Sh3 milioni. Ni wakati wa kuangazia msimu ujao,” akasema Shikanda.

Ingwe kwa sasa wanashikilia nafasi ya tatu jedwalini wakiwa na pointi 43 kutokana na mechi 23, ukiwa mwanya wa pointi saba nyuma ya vinara Tusker walio na pointi 51, huku KCB wakishikilia nafasi ya pili kwa pointi 47.

You can share this post!

Kilio cha wafugaji wa kuku Kiambu

Wagombea wa UDA, Jubilee eneobunge la Kiambaa wawarai...