• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 3:24 PM
Shughuli kama nyuki JKIA wanariadha wakianza kumiminika kwa Kip Keino Classic

Shughuli kama nyuki JKIA wanariadha wakianza kumiminika kwa Kip Keino Classic

Na AYUMBA AYODI

Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) unatarajiwa kuwa na shughuli nyingi hapo Septemba 16, huku wanariadha wengi wa kigeni wakimiminika kabla ya Riadha za Absa Kip Keino Classic hapo Septemba 18 jijini Nairobi.

Mkurugenzi wa mashindano haya Barnaba Korir amefichua kuwa karibu wanariadha 53 watatua kutoka ndege mbalimbali kuanzia mapema Alhamisi.“Kuna idadi ya wanariadha wa kigeni waliofika nchini tayari baada ya kuanza kuwasili Septemba 11,” alisema Korir aliyeahidi kuwa mashindano yatakuwa ya kufana.

Jumla ya wanariadha 265 kutoka humu nchini na ughaibuni watatifua vumbi katika duru hiyo ya kukamilisha msimu wa 2021 wa Riadha za Dunia za Continental Gold Tour ugani Kasarani.

 Kutoka idadi hiyo, 185 watashiriki vitengo vikuu na muhimu nao 80 watashiriki kitengo cha kitaifa.Bingwa mara tatu wa dunia mbio za mita 100 Justin Gatlin na Mwamerika mwenzake Bromell Trayvon, wako katika orodha ya wanariadha wanaotarajiwa kuwasili hapo Alhamisi.

Wengine walioratibiwa kutua nchini Alhamisi ni bingwa wa dunia mita 800 Narima Naakayi na bingwa wa mita 3,000 kuruka viunzi na maji wa Olimpiki Peruth Chemutai (Uganda) na Christine Mboma kutoka Botswana aliyetwaa nishani ya fedha ya mita 200 kwenye Olimpiki nchini Japan mwezi Agosti.

Mshindi wa medali ya fedha ya mita 100 Fred Kerley kutoka Amerika pamoja na bingwa wa Jumuiya ya Madola mita 400 Isaac Makwala kutoka Botswana pia watawasili Alhamisi pamoja na mshindi wa nishani ya shaba ya mita 200 ya Riadha za Dunia za Under-20 Sinesipho Dambile kutoka Afrika Kusini.

Bingwa wa Olimpiki wa fani ya uwanjani ya Hammer Throw, Wojciech Nowicki na mfalme wa mchezo huo mwaka 2017 na 2019 Pawel Fajdek (wote Poland) wanatarajiwa kuwasili Septemba 17.

Kikao rasmi na wanahabari kitaandaliwa Ijumaa katika hoteli ya Ole Sereni.

  • Tags

You can share this post!

CBC: Magoha apuuza malalamishi ya wazazi

CHARLES WASONGA: Serikali izuie wizi wa vyakula vya misaada...