• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:16 PM
Tammy Abraham aweka rekodi ya ufungaji mabao Serie A

Tammy Abraham aweka rekodi ya ufungaji mabao Serie A

Na MASHIRIKA

TAMMY Abraham aliweka rekodi ya kuwa mwanasoka wa pili raia wa Uingereza baada ya Paul Gascoigne aliyechezea Lazio mnamo 1992 kuwahi kufunga bao katika gozi la jiji la Roma huku magoli yake mawili yakisaidia waajiri wake AS Roma kucharaza Lazio 3-0 katika Ligi Kuu ya Italia (Serie A) mnamo Jumapili.

Abraham aliwaweka Roma kifua mbele katika dakika ya kwanza kabla ya kupachika wavuni bao la pili kunako dakika ya 22. Lorenzo Pellegrini alijaza kimiani goli la tatu la Roma na kuzamisha kabisa chombo cha wageni wao ugani Olimpico.

Ushindi huo wa Roma uliwawezesha kuchupa kwenye msimamo wa jedwali la Serie A hadi nafasi ya tano kwa alama 51, mbili zaidi kuliko Atalanta na Lazio.

Ni pengo la alama nane kwa sasa ambalo linatenganisha Roma ya kocha Jose Mourinho na Juventus wanaofunga orodha ya nne-bora. Zikisalia mechi nane pekee kabla ya kampeni za Serie A msimu huu kutamatika rasmi, kubwa zaidi katika maazimio ya Roma kwa sasa ni kupigania nafasi ya kuingia nne-bora ili kufuzu kwa soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) msimu ujao.

Abraham, 24, kwa sasa ndiye mwanasoka wa pili raia wa Uingereza baada ya Gerry Hitchens aliyechezea Inter Milan miaka 60 iliyopita kuwahi kufikisha mabao 14 katika Serie A.

Trevor Francis ndiye Mwingereza wa mwisho kuwahi kufunga mabao matatu katika mechi moja ya Serie A. Aliweka rekodi hiyo mnamo 1983 akivalia jezi za Sampdoria.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Jumwa kupendelea wawaniaji wa kiume kwaibua gumzo kali

Raila: Washirika wa Kalonzo sasa walegeza kamba

T L