• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 5:50 AM
Timu ya Viziwi Nakuru yajiandaa kwa mashindano ya Afrika

Timu ya Viziwi Nakuru yajiandaa kwa mashindano ya Afrika

NA RICHARD MAOSI

TIMU ya viziwi kutoka Nakuru, wanaendelea kufanya mazoezi uwanjani Afraha wakijiandaa kushiriki kwenye michuano ya bara Afrika kuanzia Tarehe 22 Mei mwaka huu.

Wachezaji hao ndio mabingwa wa kinyang’anyiro cha Majaribio ya Kitaifa kwa Wachezaji Viziwi, almaarufu kama National Deaf Trials Cup 2021, yaliyokamilika tatu zilizopita mjini Nakuru.

Michuano hiyo ilishirikisha timu tano kutoka Turkana, Kajiado, Kakamega, Siaya na wenyeji Nakuru, ambao waliibuka kidedea baada ya kushinda mechi zao zote.

Katika ngarambe hiyo , timu kutoka Siaya waliridhika na nafasi ya pili, kando na kuonyesha soka ya hali ya juu.

Nakuru walishinda baada ya kutinga fainali kukabiliana na timu ya Siaya uwanjani Afraha, baada ya kulemea wapinzani mikondo yote miwili.

Akizungumza na Taifa Leo , mkufunzi Knight Lugalya, aliwamiminia sifa wachezaji wake akisema walionyesha soka ya hali ya juu.

Alieleza kuwa kikosi chake kilistahili ushindi huo muhimu na hivi sasa kimeelekeza macho yake yote kwa mashindano ya bara Afrika mwaka huu na hatiamaye Olimpiki 2022 nchini Brazil.

Ikiwa watanya vyema katika mashindano ya Mei 2021, kikosi cha Kenya kitasafiri hadi Brazil kushiriki kwenye michuano ya Deaf Olympics ya ulimwengu.

Ingawa wachezaji wengi walikuwa na changamoto za nauli na marupurupu hawakuata tamaa katika kampeni ya kusaka taji.

Aliongezea kuwa ni wachezaji 32 ambao wameitwa kambini kuendelea na mazoezi, huku akiwaomba akinadada kujitokeza kwa wingi ili kushiriki katika mchezo wa soka.

“Hivi sasa tunajiandaa kuwakisha Kenya katia mechi ambayo itakutanisha timu kadhaa kutoka bara la Afrika kuanzia tarehe 22 mei 2021,”akasema.

Kuanzia hapo kikosi kitajiandaa kushiriki katika michuano ya Olimpiki itakayofanyika nchini Brazil mwaka wa 2022.

Mchezaji bora wa Nakuru Titus Chokalam alisema ushirikiano mzuri baina ya safu ya ulinzi na ile ya mashambulizi ulisaidia timu yake kupata ushindi.

Aidha alisema ushindani mkali wa timu zilizoshiriki ni ishara tosha kuwa kiwango cha soka nchini kinaendelea kuimarika.

You can share this post!

Pigo mkali wa Safari Rally akifariki

Watu 4 wa familia moja waangamia ajalini