• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 7:50 AM
Tutapandisha hadhi ya CAF kwa kutendea haki maandalizi ya AFCON 2027, yasema BMT

Tutapandisha hadhi ya CAF kwa kutendea haki maandalizi ya AFCON 2027, yasema BMT

MUHTASARI

  • Mashindano makubwa ya soka barani Afrika kwa nchi za Afrika Mashariki kwa mara ya mwisho yalifanyika Tanzania ambayo yalikuwa ni yale ya Mataifa ya Afrika kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U-17) 2019.

Na MASHIRIKA

MWENYEKITI wa Baraza la Taifa la Michezo Tanzania (BMT), Leodgar Tenga, amesema kuwa Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) halitojutia kuzipa Kenya, Uganda na Tanzania uenyeji wa fainali za Mataifa Bingwa Afrika (AFCON) mwaka 2027.

Alhamisi mchana, Rais wa Caf, Dkt Patrice Motsepe alitangaza kuwa maombi ya pamoja ya Kenya, Uganda na Tanzania yaliyopewa jina la Pamoja Bid yameshinda mchakato wa kuandaa fainali za AFCON 2027, yakipiku maombi ya nchi za Algeria, Senegal, Misri na Botswana.

Akizungumzia ushindi huo wa nchi hizo zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Tenga ambaye amewahi pia kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Caf na Rais wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), alisema kuwa anaamini nchi za Kenya, Uganda na Tanzania zitafanya maandalizi mazuri ambayo yatafanya AFCON 2027 iwe ya kihistoria.

“Nataka niseme tu kwamba hawatasikitika. Watafurahi kwa sababu tuna uhakika tutajitayarisha vizuri na tutaiheshimisha Caf. Na nirudie tena kuwashukuru viongozi wetu wa nchi. Viongozi wetu, Mama Samia Suluhu, Rais William Ruto, Rais Yoweri Museveni wote walikuwa nyuma yetu.

“Na walifurahi sana pale ambapo tuliwaonyesha picha zao, tumewaonyesha tulivyo na niseme wazi wamefurahi mpira na si mpira peke yake, wamefurahia nje, jinsi ambavyo watakwenda mbuga za wanyama maana yake tumewaambia sisi ni watu wakarimu,” alisema Tenga.

Tenga alishauri pia kufanyike kila kinachowezekana ili maandalizi yafanyike vizuri kuthibitisha kwamba Kamati ya Utendaji ya Caf haikukosea kuzipa Kenya, Uganda na Tanzania uenyeji wa fainali za AFCON 2027.

Ikumbukwe hii ni mara ya kwanza kwa fainali za AFCON kuandaliwa na nchi za Kenya, Uganda na Tanzania.

  • Tags

You can share this post!

Wanaharakati washinikiza karani wa Bunge la Kaunti ya...

Mtangazaji wa redio King Kalala: Nimepatana kimwili na...

T L