• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 9:55 AM
Ubelgiji yazamisha Belarus na kufungua mwanya wa alama tisa kileleni mwa Kundi E

Ubelgiji yazamisha Belarus na kufungua mwanya wa alama tisa kileleni mwa Kundi E

Na MASHIRIKA

KIUNGO Dennis Praet alifunga bao la pekee na la ushindi na kusaidia timu ya taifa ya Ubelgiji iliyokosa huduma za wanasoka wengi wa haiba kubwa kucharaza Belarus 1-0 katika mechi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia na hivyo kufungua pengo la alama tisa kileleni mwa Kundi E.

Chini ya kocha Roberto Martinez, Ubelgiji kwa sasa wanajivunia alama 16 kutokana na mechi sita. Mgongo wa kikosi hicho kinachoorodheshwa cha kwanza dunini kwa mujibu wa viwango bora vya Shirikisho la Soka Kimataifa (FIFA), unasomwa na Jamhuri ya Czech pamoja na Wales ambao wana alama saba kila kila mmoja.

Wales ambao wamecheza mechi nne, waliambulia sare tasa dhidi ya Estonia ambao sasa wanavuta mkia kwa alama moja kutokana na michuano minne. Ni pengo la pointi nne ndilo linatamalaki kati ya nambari nne Belarus na Wales wanaoorodheshwa wa tatu nyuma ya Jamhuri ya Czech kwa sababu ya uchache wa mabao.

Ubelgiji walishuka dimbani kuvaana na Belarus jijini Kazan, Urusi bila kujivunia huduma za wachezaji Romelu Lukaku, Axel Witsel, Thibaut Courtois na Thomas Meunier.

Kocha Martinez alimsaza benchi kiungo na nahodha Eden Hazard hadi dakika 30 za mwisho alipoletwa ugani kujaza pengo la Leandro Trossard. Kutokana na mabadiliko hayo makubwa kikosini mwao, Ubelgiji walikosa kasi na makali yaliyowashuhudia wakipepeta Belarus 8-0 katika mchuano wa mkondo wa kwanza mnamo Machi 2021 jijii Brussels.

Bao la Praet ambaye huchezea Torino ya Ligi Kuu ya Italia (Serie A) lilikuwa zao la ushirikiano mkubwa kati yake na fowadi matata wa AC Milan, Alexis Saelemaekers.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO 

You can share this post!

AKILIMALI: Huzifikirii sana chupa za plastiki ila kwake ni...

Kipchoge azindua wakfu, alenga kuwapa watoto maarifa