• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 8:55 AM
Uchunguzi wa mauaji ya Damaris waanza

Uchunguzi wa mauaji ya Damaris waanza

Na GEOFFREY ANENE

JAMII ya riadha na michezo kwa jumla Jumatano iliendelea kuomboleza kifo cha mwanariadha Damaris Muthee Mutua aliyepatikana ameuawa katika eneo la Iten, Kaunti ya Elgeyo-Marakwet mnamo Aprili 19.

Mutua, 28, ambaye kimataifa anawakilisha Bahrain baada ya kubadili uraia, anaaminika kuuliwa na mpenzi wake wa kiume Eskinder Hailemaryam Folie.

Polisi wanasaka raia huyo wa Ethiopia ambaye pia vyombo vya habari vimemtaja kama Koki Fai.

Anasemekana ametorokea nchini mwake.

Hapo jana Jumatano, kocha Gregory Kilonzo alisema kuwa Mutua, ambaye ni mzawa wa kaunti ya Machakos, alifanya mazoezi vyema katika kambi ya timu ya taifa ya Bahrain mjini Kapsabet, kaunti ya Nandi mnamo Jumamosi iliyopita.

“Hatukumuona Jumapili wala Jumatatu na kulazimika kumtafuta kwake Iten baada pia kukosa kumpata kwenye simu yake mnamo Jumanne asubuhi. Tulipata nguo zake tu. Baadaye siku hiyo tulipata habari kuwa ameuawa katika nyumba na mwanariadha huyo kutoka Ethiopia,” alisimulia Kilonzo ambaye pia ananoa mastaa kama bingwa wa Olimpiki 2016 mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji Ruth Jebet na bingwa wa dunia wa marathon duniani mwaka 2017 Rose Chelimo.

Aidha, bei ya tiketi za riadha za kimataifa za Kip Keino Classic imetangazwa.

Mashabiki watalipa Sh200 langoni kufurahia uhondo huo ugani Kasarani mnamo Mei 7.

  • Tags

You can share this post!

Raila asukumwa na washirika wake

Washukiwa watatu wa mauaji ya mwanafunzi wa JKUAT kusalia...

T L