• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 6:39 PM
Ufaransa wazima matumaini ya vipusa wa Iceland kutinga robo-fainali za Euro 2022

Ufaransa wazima matumaini ya vipusa wa Iceland kutinga robo-fainali za Euro 2022

Na MASHIRIKA

WAREMBO wa Iceland waliaga kipute cha Euro 2022 baada ya kulazimishiwa sare ya 1-1 na Ufaransa mnamo Jumatatu usiku uwanjani New York, Uingereza.

Matokeo hayo yaliwezesha Ufaransa kukamilisha kampeni zao kileleni mwa Kundi D kwa alama saba, nne zaidi kuliko Ubelgiji waliopepeta Italia 1-0. Iceland walikamata nafasi ya tatu kundini kwa pointi tatu, mbili zaidi kuliko Italia.

Dagny Brynjarsdottir alisawazishia Iceland kupitia penalti ya dakika ya 12 baada ya Melvine Malard kuwaweka Ufaransa uongozini katika dakika ya kwanza.

Straika wa Ufaransa Melvine Malard (wa pili kulia) afunga bao la kwanza la Ufaransa kwenye mechi yao dhidi ya Iceland uwanjani New York mjini Rotherham, Uingereza, Julai 18, 2022. PICHA | AFP

Mechi hiyo ilihudhuriwa pia na kocha wa Uholanzi, Mark Parsons, ambaye sasa ataongoza warembo wake kumenyana na Ufaransa katika hatua ya robo-fainali mnamo Julai 23, 2022.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Warembo wa Ubelgiji wapepeta Italia na kufuzu kwa...

Kihara atakiwa kujibu Sonko katika korti ya Afrika Mashariki

T L