• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 8:55 PM
Warembo wa Ubelgiji wapepeta Italia na kufuzu kwa robo-fainali za Euro kwa mara ya kwanza katika historia

Warembo wa Ubelgiji wapepeta Italia na kufuzu kwa robo-fainali za Euro kwa mara ya kwanza katika historia

Na MASHIRIKA

VIPUSA wa Ubelgiji walitinga robo-fainali za Euro 2022 kwa mara ya kwanza katika historia baada ya kupepeta Italia 1-0 katika mchuano wa Kundi D uliowakutanisha ugani Academy, Uingereza mnamo Jumatatu usiku.

Bao la pekee na la ushindi katika mechi hiyo lilifumwa wavuni na Tine de Caigny katika dakika ya 49. Chini ya kocha Ives Serneels, Ubelgiji sasa watavaana na Uswidi katika hatua ya nusu-fainali mnamo Julai 22, 2022.

Italia waliopoteza nafasi nyingi za wazi kupitia kwa Cristiana Girelli walidenguliwa kwenye Euro 2022 baada ya kupoteza mechi mbili kati ya tatu kundini.

Hii ni mara ya pili kwa Ubelgiji wanaoshikilia nafasi ya 19 duniani kunogesha kipute cha Euro. Sasa watakuwa na kibarua kizito dhidi ya nambari mbili duniani, Uswidi, katika gozi la nne-bora uwanjani Leigh Sports Village.

Ubelgiji wanafuzu kwa robo-fainali baada ya kukamilisha kampeni za Kundi D katika nafasi ya pili kwa alama nne, tatu nyuma ya viongozi Ufaransa. Iceland waliambulia nafasi ya tatu kundini kwa alama tatu, mbili zaidi kuliko Italia waliotinga robo-fainali za Kombe la Dunia mnamo 2019.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Zlatan Ibrahimovic atia saini mkataba mpya wa mwaka mmoja...

Ufaransa wazima matumaini ya vipusa wa Iceland kutinga...

T L