• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Uingereza kuwakilishwa na vikosi vinane kwenye soka ya bara Ulaya 2023-24

Uingereza kuwakilishwa na vikosi vinane kwenye soka ya bara Ulaya 2023-24

Na MASHIRIKA

UINGEREZA itakuwa na wawakilishi wanane kwenye vipute vitatu vya soka ya bara Ulaya msimu ujao wa 2023-24.

Newcastle United waliambulia nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo 2022-23 baada ya kujizolea jumla ya alama 71.

Ufanisi huo uliwapa tiketi ya kunogesha UEFA pamoja na Manchester United, Arsenal na Manchester City waliotia kapuni alama 75, 84 na 89 mtawalia.

Liverpool na Brighton walifuzu moja kwa moja kivumbi cha Europa League baada ya kumaliza kampeni ya EPL katika nafasi ya tano na sita kwa alama 67 na 62 mtawalia.

Kikosi kingine cha EPL kilichofuzu kwa kipute hicho cha Europa League ni West Ham United waliopepeta Fiorentina ya Italia 2-1 kwenye fainali ya Europa Conference League mnamo Juni 7, 2023 jijini Prague, Jamhuri ya Czech.

Aston Villa walioambulia nafasi ya saba kwenye msimamo wa jedwali la EPL kwa alama 61, walifuzu kwa dimba la Europa Conference League mnamo 2023-24.

Kabla ya ushindi wa West Ham dhidi ya Fiorentina, idadi ya juu zaidi ya vikosi vya Uingereza ambavyo vingenogesha soka ya bara Ulaya muhula ujao wa 2023-24 ilikuwa saba. Klabu hizo zilikuwa zifuzu kwa vipute UEFA, Europa League au Europa Conference League kutokana na ubora wa matokeo yao ligini, kwa kushinda Kombe la FA au Carabao Cup.

KLABU BINGWA ULAYA (UEFA): Man City, Arsenal, Newcastle United, Manchester United.

EUROPA LEAGUE: Liverpool, Brighton, West Ham United.

EUROPA CONFERENCE LEAGUE: Aston Villa.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Ruto, Raila wapongeza Faith Kipyegon kwa kuweka rekodi mpya...

Mahakama yamuonya mzungu aliyedai wakuu serikalini ni...

T L