• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 6:39 PM
Madai ya usimamizi mbaya, ubadhirifu FKF ni pigo kwa michezo nchini

Madai ya usimamizi mbaya, ubadhirifu FKF ni pigo kwa michezo nchini

Na GEOFFREY ANENE

KATIBU wa Shirikisho la Mpira wa Magongo Kenya (KHU) Wycliffe Ongori anasema kesi zinazokabili viongozi wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF) ni pigo kwa michezo mingine humu nchini.

Ongori, ambaye alichezea Kenya kimataifa na klabu ya Wazalendo katika fani ya mpira wa magongo miaka ya 90 na 2000 kama mshambuliaji, alieleza Taifa Leo kuwa kesi hiyo, ambayo imeshuhudia rais wa FKF Nick Mwendwa na Afisa Mkuu Mtendaji Barry Otieno wakitiwa nguvuni na kushtakiwa, inaharibia klabu na mashirikisho mengine kutafuta usaidizi kutoka kwa serikali.

Mwendwa anakabiliwa na kesi ya kutumia mamlaka yake vibaya, kuendesha shirikisho hilo vibaya pamoja na kutumia mamia ya milioni ya fedha kutoka kwa serikali vibaya. Amekuwa akichunguzwa na maafisa wa jinai (DCI) na anatarajiwa kufikishwa kortini mnamo Novemba 15, 2021.

Katika mahojiano na afisa huyo wa KHU, amesema Jumatatu, “Maoni yangu kuhusu suala hili lote ni kuwa si kitu kizuri kabisa kwa michezo. Natamani tungekuwa tunatumia muda huu kuimarisha viwango vyetu vya michezo na usimamizi wa michezo. Huenda matukio ya FKF hayatuathiri moja kwa moja wakati huu, lakini yanachangia kwa njia moja ama nyingine kufanya usaidizi kuwa mgumu,” alisema Ongori.

You can share this post!

Wezi wa mali ya umma tutawatia adabu – Moi

WANTO WARUI: Migomo shuleni ichunguzwe vilivyo kubaini...

T L